Moshi ukiwa unazidi katika eneo ambalo maduka matatu yameteketea kwa moto.
Mashuhuda wakiwa wameanza kuelekea eneo la tukio
Moto ukiwa unaanza kupamba moto, waya wa umeme unao onekana unashuka chini ndio umesababisha moto huo.
Moto ukiwa unazidi pamba moto katika duka la kushonea nguo na kuuza vitambaa.
Baadhi ya Vijana wasamalia wema wakiondoa mabati ili kuzuia moto usiendelee kuwaka zaidi.
Sehemu ya nyaya za umeme uliosababisha moto huo.
Baadhi ya Mashuhuda wakimwagiwa maji kupisha njia ya waokoaji waliojitolea kuzima moto.
Mmoja wa Mashuhuda akiwa anachukua tukio kwa umakini
Kikosi cha zima moto wakiwasili eneo la tukio, huku wananchi wakiwazuia wasifanye kazi aada yakuwasili na kukuta wananchi hao wameshajitolea kuuzima moto huo.
Kikosi cha zima moto wakianza shuguli ya kumalizia kuzima moto.
Maji ya kuwasha yakiwa yamefunguliwa ili kuwatawanya watu wasikae mbele kupisha kazi ya kuzima moto.
Kikosi maalum cha kuzuia vurugu cha Jeshi la Polisi (FFU) wakiwa wamefika eneo la tukio kwa ajili ya kulinda usalama
TANESCO wakiwa wamefika eneo la tukio
Vijana wakiwa wanalalamikia kikosi cha zima moto kuwa wamechelewa kufika eneo la tukio na kuzima moto.
Watu wakiwa wanazidi kuzuiliwa kupisha kazi ya uokoaji.
Kikosi maalum cha zima moto wakiwa wanamalizia kazi ya kuzima moto kidogo uliobakia
Kila mtu anajitahidi kupata tukio
Kazi ikiwa inaelekea kumalizika
Baadhi ya mabaki uya mabati.
Kazi ya kuzima moto ikiwa imeisha , mmoja ya wanakikosi cha wazima moto akiwa anafunga mtambo
Hivi ndivyo maduka yalivyobakia pamoja na nyumba iliyo ungua
Mabaki ya vitu katika duka la vitambaa ya nguo na ushonaji
Mmoja ya wanakikosi cha zimamoto akiwa anaongea na wananchi
Wananchi wa mwananyamala wakiwa wanasikika wakisema "Wamekuja zima moshi... wamekuja zima moshi..."
Mmoja wa wazee wa Mwananyamala Mussa Kisoki, Kisoki, akizungumza na waandishi wa habari.
Mmoja wa mashuhuda akiwa anaelezea jinsi moto ulivyotokea na kushukuru wananchi na Kikosi cha kuzima moto kwa kazi kubwa iliyofanikisha zoezi la kuzima moto.
Kazi ikiwa imeisha hizi ndizo ndoo ambazo zilisaidia kwa kiasi kikubwa kuchota maji na kuzima moto pamoja na baadhi ya vijana wachache walio saidia kuzima moto huo.
No comments:
Post a Comment