Habari za Punde

*MSHAMBULIAJI WA BRAZIL SANTOS ATUA KUJIUNGA NA MWENZIE COTINHO KUIPA MAKALI YANGA

 Mshambuliaji mpya Yanga, Geilson Santana Santos ‘Jaja’ (kulia) akipunga mkono kuwasalimia mashabiki wa Yanga waliokuwepo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana wakati alipowasili akitokea nchini kwao Brazil kuja kujiunga na Klabu ya Yanga. Santos ni Mbrazil wa pili kutua nchini kujiunga na Yanga akiungana na Kiungo mshambuliaji aliyekwishaanza mazoezi na Yanga, Coutinho.
Sehemu ya mashabiki, waandishi wa habari na viongozi wa Yanga, waliofika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere kumpokea mshambuliaji huyo jana. 
***********************************
Mshambuliaji huyo pia hakuweza kuzungumza na Waandishi wa Habari kutokana na kuzungumza Lugha ya Kireno pekee na hapakuwepo na mkalimani uwanjani hapo.
Mpaka sasa Klabu ya Yanga SC ina jumla ya wachezaji watano wa kigeni kabla ya Santos ambapo tayari kuna tetesi kuwa Klabu hiyo ina mpango wa kumtema Mganda Emmanuel Okwi.

Wachezaji wengine wa Kigeni walio ndani ya Klabu hiyo mpaka sasa ni pamoja na beki Mbuyu Twite, kiungo Haruna Niyonzima wote wa Rwanda, Hamisi Kiiza na Coutinho.

'Jaja' amezaliwa Septemba 21 mwaka 1985 (28) mjini Aracaju, Brazil na ametokea katika klabu ya Itabaiana aliyojiunga nayo mwaka 2006 na kabla ya hapo aliwahi kuzichezea klabu za Coritiba, Catuense, Olimpico, zote mwaka 2013, Maruinense, Lagarto mwaka 2012, Olimpico tena 2011, Domingos 2010, Confianca 2008 na Sergipe 2007.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.