Na Sufianimafoto
Reporter, Dar
KIUNGO
mpya wa Yanga Mbrazil, Andrey Coutinho, amewataka mashabiki wa Klabu hiyo na
wanachama kuondoa hofu na kusubiri kupata raha na burudani ya soka kutoka kwa
Klabu yao, iliyoanza mazoezi ya kujiandaa na Ligi kuu Bara msimu wa 2014-2015 na
ile ya Shirikisho.
Kiungo huyo
aliyekabidhiwa Jezi namba 7, iliyokuwa ikivaliwa na Mshambuliaji Mburundi,
Didier Kavumbagu aliyetimkia Azam Fc, amesaini mkataba wa miwaka miwiki
kuitumikia Klabu hiyo.
Mbali na Kiungo huyo,
pia Uongozi wa Yanga umemtuma mmoja kati ya viongozi wake kukwea Pipa kuelekea
Brazil kwa ajili ya kunasa wachezaji kadhaa alioelekezwa na kocha mpya wa
Yanga, Marcio Maximo, ili mmoja kati yao aweze kutua Bongo kujiunga na Klabu
hiyo.
Maximo
amewapa Yanga SC mawasiliano ya wachezaji kadhaa wa Kibrazil wanaocheza nchini
humo, ili waweze kuonana na viongozi wa Yanga wakitua nchini humo na iwapo wakiridhishwa
na viwango vyao waweze kufanya mchakato wa kutua nao nchini.
Ujio
wa Kiuongo huyo na iwapo atatua Mbrazil mwingine katika kikosi hicho, Yanga SC itakuwa
ikitimiza mpango wake wa kuachana na Mganda mmoja wapo kati ya Hamisi Kiiza au
Emmanuel Okwi, kwa kuwa idadi ya wachezaji wa kigeni katika Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara mwisho ni watano tu.
Wachezaji wageni waliokwisha saini mkataba Yanga ni beki Mbuyu Twite, kiungo Haruna Niyonzima kutoka Rwanda, Coutinho wa Brazil, Kiiza na Emmanuel Okwi wote wa Uganda- maana yake ili kuongeza mchezaji mwingine wa kigeni itatakiwa kupunguza mmoja, ambapo na Diego wa Kampala yuko kwenye mstari mwekundu.
Wachezaji wageni waliokwisha saini mkataba Yanga ni beki Mbuyu Twite, kiungo Haruna Niyonzima kutoka Rwanda, Coutinho wa Brazil, Kiiza na Emmanuel Okwi wote wa Uganda- maana yake ili kuongeza mchezaji mwingine wa kigeni itatakiwa kupunguza mmoja, ambapo na Diego wa Kampala yuko kwenye mstari mwekundu.
Yanga
SC imekwishaanza mazoezi rasmi chini ya makocha wake wapya, Wabrazil Marcio
Maximo na Msaidizi wake, Leonardo Neiva, asubuhi ikijifua katika fukwe za Coco
na jioni Uwanja wa Chuo cha Bandari, Tandika jijini Dar es Salaam.
Yanga
SC inatarajia kushiriki Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu
kama Kombe la Kagame mwezi ujao mjini Kigali, Rwanda na ikirudi itafungua pazia
la msimu wa Ligi Kuu kwa kumenyana na mabingwa Azam FC katika mechi ya Ngao ya
Jamii mwezi huo huo.
Na
baadaye mapema mwakani, Yanga SC iliyomaliza nafasi ya pili msimu uliopita
katika Ligi Kuu, itashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

No comments:
Post a Comment