Habari za Punde

*RAIS KIKWETE AFUNGUA RASMI UKUMBI WA MIHADHARA WA CHUO CHA SEKOMU

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Mkuu wa Chuo cha Sebastian Kolowa Memorial University SEKOMU  Askofu Dr.Stephen Munga(kushoto)Makamu Mkuu wa Chuo cha SEKOMU Dr.Anneth Munga(watatu kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Galawa(kulia) wakikata utepe kuzindua rasmi ukumbi wa mihadhara wa Benjamin William Mkapa wilayani Lushoto jana.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha wageni muda mfupi baada ya kuwasili katika Chuo Kikuu chA Sebastian Kolowa Memorial University mabapo alifungua ukumbi wa mihadhara na kuhutubia wananchi.Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha SEKOMU Askofu Dr.Stephen Munga na kulia ni makamu wa chuo Dr.Anneth Munga.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasililiza kwa makini wanafunzi kutoka Irente school for the Blind wakati walipoimba shairi maalumu wakati wa sherehe za ufunguzi wa ukumbi wa mihadhara wa Benjamin William Mkapa katika  chuo kikuu cha Sebastian Kolowa Memorial University SEKOMU jana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wanafunzi wa wageni waliohudhuria sherehe ya ufunguzi wa ukumbi wa mihadhara wa Benjamin William Mkapa uliofanyika katika chuo kikuu cha Sebastian Kolowa Memorial University SEKOMU huko Lushoto Mkoani Tanga jana. Picha na Freddy Maro

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.