Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Wabunge wa Lushoto Mhe.Henry Shekifu kushoto na mbunge wa Bumbuli Mhe.January Makamba(kulia) muda mfupi baada ya Rais kuhutubia wananchi katika mkutano wa hadhara Jimbo la Bumbuli Wilayani Lushoto jana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Usambara schools wakati aliposimama na kuwasalimia huko Lushoto jana ambapo alikagua miradi ya maendeleo na kuhutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Nyerere square mjini Lushoto jana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhi ufunguo kwa mmoja wa wakulima waliokopeshwa matrekta kwaajili ya kilimo wilyani Lushoto jana.
******************************************
JK. AMFAGILIA JANUARY MAKAMBA BUMBULI
*Ampongeza kwa uwezo wake
*Amsifia kwa uwajibikaji wake
''January anafanya kazi nzuri ya Ubunge. Pia ananisaidia sana kwa kazi ya Wizara niliyompa. Unajua January alipogombea Ubunge alinificha. Nilikuwa nasikia kwa wenzake tu pale ofisini.
Baadaye alivyoweka mambo yake sawa ndio akaja kuniambia kwamba Mzee na Mimi najitosa. Nikamtakia heri. Kwa kweli kwa jinsi anavyohangaika na Jimbo lake inaonyesha Ubunge aliutaka Kwa dhati kabisa ya kusaidia watu wa Bumbuli. Nimesikia anafikiria mambo makubwa. Hajaniambia. Mi Nimesikia tu. Namtakia kila la heri.
Haya mambo anaamua Mungu. Wala hayalazimishwi. Mungu akitaka linakuwa hata kama watu wote hawataki. Mungu akiwa hataki hata kama mtu ukitaka jambo hilo vipi haliwezi kuwa. Mimi nilishauriwa na Mzee mmoja kwamba jambo likifika wakati wake utalipata hata kama utapingwa kiasi gani. Kama halijafika wakati wake haliwezi kutokea.
Mimi niligombea 1995 sikupata kwasababu haikuwa wakati wake. 2005 ikawa wakati wake nikapata. Na wewe usipopata sasa usiweke nongwa"



No comments:
Post a Comment