Habari za Punde

*RAIS KIKWETE AKAGUA KILIMO CHA KAHAWA MBINGA LEO.

 Meneja wa Shamba la Kahawa la AVIV Farm linalomilikiwa na kampuni ya Olam Bwana Medappa Ganapati akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mche bora wa kahawa iliyozaa vyema wakati Rais alipolitembelea na kukagua shamba la kahawa katika kijiji cha Lipokela, wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua Soko la Kimataifa la Mkenda lililopo katika kijji cha Mkenda Mpakani mwa Msumbiji na Tanzania leo.kulia ni mbunge wa Peramiho Mh.Jenister Mhagama.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi miche bora ya kahawa mkulima mdogo Bi Dorothea Komba wakati alipolitembelea na kukagua shamba la kahawa AVIV Farm linalomilikiwa na kampuni ya Olam katika kijiji cha Lipokela wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma leo.Kampuni ya Olam imepanga kutoa jumla ya miche milioni tatu kwa wakulima wadogo elfu mbili katika vijiji vinne vinavyozunguka shamba hilo katika kipindi cha miaka mitano ili kuwashirikisha kuzalisha kahawa bora.
 Rais Jakaya Kikwete mpenda watoto, akiwa amembeba mtoto.....Picha na Fredy Maro

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.