NA MAGRETH KINABO. MAELEZO
TATIZO la kutokuwepo umeme katika jijini Dares Salaam hususan maeneo ya katikati ya mji na nje kidogo ya mji na mkoa wa Arusha, ikiwemo mikoa ya Mwanza na Shinyanga linatarajiwa kupatiwa ufumbuzi ifikapo Juni mwaka 2015.
Hayo yalisemwa leo na Mhandisi Mkuu wa masuala ya Umeme kutoka Benki ya Maendeleao ya Afrika(ADB), Dkt. Babu RAM wakati akizungumza na waandishi wa habari leo(jana) mara baada ya Waziri wa Fedha wa Marekani , Jack Lew ambaye aliwasili nchini usiku wa kuamkia leo(jana) na alitembelea nchini, jijini Dares Salaam kwa ziara ya siku moja ili kujionea shughuli mbalimbali ukiwemo mradi wa ‘Electricity V ‘ unaoendelea kwenye Kituo kidogo cha kusambazia umeme kilijulikanacho kwa jina la Sokoine.
“ Mradi huu ni mojawapo ya agenda ya Serikali ya Tanzania ya matokeo makubwa sasa(BRN). Unahusisha ujenzi na uboreshaji wa vituo vidogo vya umeme vilivyoko katika jiji la Dar es Salaam na mkoa wa Arusha, pia unahusisha upanuzi wa miundombinu ya usambazaji wa umeme katika mikoa ya Mwanza na Shinyanga. Unaratajia kukamilika katikati ya mwaka 2015,” alisema RAM.
Alisema mradi huo katika kituo hicho , ambacho kinahusisha jiji la Dares Salaam na mkoa wa Arusha kinatarajia kunufaisha mara mbili ya idadi ya sasa ambao ni wateja 3000 na wafanyabiashara wakubwa 400. Pia wateja usambazaji wa umeme katika mikoa ya Mwanza na Shinyanga utanufaisha wateja wapya 9000.
“Mradi wote huu utanufaisha wateja wanakadriwa kufikia 12,000 na utagharimu Dola za Marekani milioni 50,” alisisitiza.
Alisema mradi huo utahusisha usambazaji wa umeme katika kituo kidogo cha umeme cha Ilala na mkoa wa Arusha kwenye eneo la Njiro.
Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa masuala ya umeme (nishati) kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Innocent Luoga alisema mradi huo ni maojwapo wa Dira ya Maendeleo ya nchi ili ifikapo mwaka 2025 Tanzania iwe ni nchi ya kipato cha kati.
Aliongeza kwamba mradi huo, utaongeza upatikanaji wa umeme kwenye maeneo ya katikati ya jiji la Dares Salaam, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Hospitali ya Ocean Road na Ikulu kwa sasa mahitaji ni makubwa kutokana na kuongezeka kwa majengo na jiji hilo kupanuka.
“Lengo kubwa la mradi huu ni mkakati wa Serikali wa kuongeza upatikanaji wa umeme katika jiji la Dares Salaam, Arusha,Mwanza,Shinyanga na maeneo ya vijijini,” alisema Luoga.
Luoga alisema katika mradi huo, itawekwa transforma yenye uwezo mkubwa wa kufikia 30MVA badala ya 15MVA zilizokuwepo hapo awali.
Alisema mradi huo unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika, ambayo inapata fedha kutoka Marekani kupitia mpango wa Rais wa Marekani, Barrack Obama wa miradi ya umeme (Power Africa Initiative),
Aliitaja miradi mingine, kuwa ni City Center unaofadhiliwa na Finland, Gongolamboto, Kurasini, Mkuranga, Mbagala, Kurasini, Kigamboni, Masaki, Mbezi, Ilala na Ubungo , ambapo itahusu upanuzi wa vituo na kuongeza transforma kubwa.
Katika ziara ya Waziri wa Fedha wa Marekani, Lew pia alitemblea Wizara ya Fedha ,ambapo alifanya mazungumzo na Waziri wa Fedha, Saada Salum Mkuya, maeneo ya Bandari . kituo cha mafuta cha Kurasini na kufanya mazungumzo na viongozi husika.
Waziri huyo amefanya ziara hiyo katika nchi za Afrika ,ambazo ni Misri, Tanzania na Afrika ya Kusini , ambapo anatarajia kuwasili nchini humo baada ya kuondoka nchi leo usiku.
Lengo la ziara hiyo ni kuhimarisha uhusiano na nchi za Afrika kupitia baada ya ziara ya Rais wa Marekani, Barrack Obama aliyoifanya mwaka jana katika nchi za Afrika na kuzindua mpango huo.
Waziri huyo atarejea nchini kwake baada ya ziara ya Afrika Kusini.
Mradi huo katika awamu ya kwanza umehusisha nchi zingine ambazo ni Kenya, Ethiopia,Ghana,Liberia na Nigeria, ikiwemo Tanzania na una lengo la kunufaisha wateja zaidi ya milioni 60.
No comments:
Post a Comment