Habari za Punde

*PESA ZA ESCROW ZITO NAE YUMO, ALIPULIWA NA RAFIKI YAKE KIPENZI, LUSINDE

Hii ndiyo barua iliyoandikwa na zito kwa ajili ya kukopa fedha hizo za Escrow kumpeleka mama yake india kutibiwa. Barua hii iliyo na vithibitisho kadhaa pamoja na kopi ya leseni ya aliyetumwa iliwasilishwa na Mbunge Lusinde Bungeni na kusomwa kisha kuikabidhi meza kuu kwa ajili ya kufanyiwa kazi.
Lusinde akichangia wakati wa mjadala huo ukiendelea Bungeni jana jioni huku akionyesha barua hiyo inayomhusisha Zito katika kashfa hiyo.
Lusinde akiendelea kuchangia huku akiwavunja mbavu wabunge kwa vijembe vyake.
Mbunge Kafulila, akichangia kujaribu kuthibitisha ukweli wa sakata hilo.
Kafulila akiendelea kumwaga nondo.
Mbunge, Joshua Nassari, akisimama kuomba mwongozo, jambo lililomfanya mwenyekiti wa kikao hicho, Zungu kuingilia kati na kupiga marufuku wabunge kuomba mwongozo wakati mmoja wao akiendelea kuchangia, kutokana na kuchelewesha muda.
Sehemu ya wabunge waliohudhuria kikao hicho cha jana jioni.
Haya ni baadhi ya majina ya waliolipwa fedha hizo na benki ya Mkombozi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.