Habari za Punde

*BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA ATEMBELEA WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kulia) akiwa katika mazungumzo na ugeni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania uliomtembelea leo Ofisini kwake ukiongozwa na Balozi Lu Youqing  (kushoto)  kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya China na Tanzania katika kuimarisha  shughuli za Mipango Miji ,Usimamizi wa Matumizi endelevu ya Ardhi . 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Alphayo Kidata  (kushoto) akifurahia jambo wakati akizungumza na ugeni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania ulioitembelea  Wizara hiyo leo jijini Dar es salaam kwa lengo la kuendeleza ushirikiano kati ya China na Tanzania katika  Matumizi endelevu ya Ardhi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kulia)  akimweleza  Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing  (kushoto) namna Wizara yake  inavyoendelea  kuimarisha  shughuli za Mipango Miji ,Usimamizi na Matumizi endelevu ya Ardhi katika maeneo mbalimbali nchini.Mkurugenzi wa Mipango  Miji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Michael Mwalukasa akifafanua jambo kuhusu mipango mbalimbali inayotekelezwa na Tanzania katika kuimarisha matumizi endelevu ya Ardhi wakati wa ziara fupi ya Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing   aliyoifanya katika wizara hiyo leo jijini Dar es salaam. Wengine wanaoonekana ni Kamishna wa Ardhi nchini Dkt. Moses Kusiluka  na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Alphayo Kidata  (kulia). Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.