Vijana wanne waliodaiwa kuwa ni majambazi wakiwa chini ya ulinzi wakiwa wamefungwa pingu baada ya kukamatwa maeneo ya Mataa ya Red Cross Upanga jijini Dar es Salaam, mchana huu. Vijana hao imeelezwa kuwa walimpora pesa raia wa kigeni (mzungu) eneo la Benki ya Stanbic iliyopo maeneo ya Kinondoni karibu na Ubalozi wa Ufaransa na kukimbia, ambapo jamaa mmoja aliyekuwa barabarani akishuhudia tukio hilo aliamua kujitolea kuwakimbiza na kufanikiwa kuwaziba alipofika kwenye Taa za Red Cross, na kufanikiwa kuwekwa chini ya ulinzi na askari Polisi wa Pikipiki waliokuwa eneo hilo. Vijana hao walikutwa na Bunduki na hikuelezwa idadi ya bunduki hizo wala kiasi cha pesa walizokuwa wamepora.
Eneo la tukio walipokamatiwa majambazi hao.
Vijana hao wanatashati wanaopendeza kwa pesa za matukio ya ujambazi wakiwa chini ya ulinzi. Picha kwa Hisani ya Mdau aliyekuwepo eneo la Tukio




No comments:
Post a Comment