Habari za Punde

*MATUKIO KATIKA PICHA MTANANGE WA YANGA v/s ETOILE DU SAHEL, MCHEZAJI TEGEMEO WA ETOILE ATAPIKA UWANJANI KABLA YA MECHI

 Mshambuliaji wa hatari wa timu ya Etoile Du Sahel, Bounedjah Baghdad, akitapika uwanjani dakika chache kabla ya kuanza mchezo wa Kombe la Shirikisho kati yao na Yanga, uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. 

Tukio hilo lilizua kizazaa kwa viongozi wa timu hiyo ambao walionekana kupagawa uwanjani hapo huku wakihaha muda wote kutafuta jinsi ya kumsaidia huku jamaa huyo akibadilika rangi na kuwa mwekundu, hadi alipopatiwa dawa na kumeza kisha kujimwagia maji na kuingia uwanjani kuanza mchezo huo.

Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare kwa kufungana bao 1-1, bao la Yanga likifungwa na Nahodha wake Nadir Haroub 'Canavaro' kwa mkwaju wa penati katika dakika ya pili baada ya Simon Msuva kuchezewa rafu katika eneo la hatari.  Bao la Etoile lilifungwa na Ben Amor Med Amine, katika dakika ya 47.
 Viongozi wa Etoile, wakimsaidia na kumpa huduma ya kwanza mchezaji wao Baghdad, wakati akiendelea kutapika. Haikuweza kufahamika kwa haraka sababu za mchezaji huyo kuanza kutapika ghafla uwanjani hapo kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
 Bahgad, akimeza dawa......
 Katika tukio jingine la kuvutia uwanjani hapo wakati wa Mtananage huo, lilikiwa ni hili la Msemaji wa Yanga, Jerry Muro, ambaye akikwenda kuketi upande wa Jukwaa la mashabiki wa Simba waliokuwa wakiishangilia Etoile, na kuzua taflani kubwa baina yake na mashabiki jambo lililowafanya askari kuingilia kati. Kama inavyoonekana pichani akibishana na mashabiki hao.
 Askari wakijaribu kumtafadhalisha Muro kuondoka eneo hilo, bila mafanikio kwani Muro aligoma na kuendelea kuketi eneo hilo huku akiwa ameweka 'spika za simu' masikioni akionyesha kutowajali wala kuwasikiliza.
 Mjadala ukioendelea pande hizo......
 Mchezaji tegemeo wa Etoile, Bounedjah Baghdad, aliyekuwa akitapika uwanjani, akichuana na Mbuyu Twite, kuwania mpira.
 Mchuano ukiendelea huku wachezaji wengine wa Yanga wakifika kutoa sapoti....
 Mrisho Ngassa, akimtoka beki wa Etoile......
 Ngassa, akichezewa rafu na beki wa Etoile....
 Kuonyesha kuwa Waarabu ni wakorofi katika mipango ya nje na ndani Kisoka, huwa hawajali hata kama wapo ugenini. Mcheki hapa Kocha mkuu wa Etoile, Benzarti Faouzi, akivuka eneo lake na kukaribia eneo la mshika kibendera huku akiwafokea wachezaji wake. Jambo hili lingefanywa na Kocha mzawa katika Ligi Kuu Bara ama Kocha wa Yanga katika mchezo huu, angepewa kadi nyekundu na kuondolewa benchini. Hili pia lilijidhihirisha pale mchezaji wa Etoile, alipokokota mpira kutoka nje ya mstari na kuendelea kucheza huku mshika kibendera akiwa eneo hilo bila kuinua kibendera jambo lililowafanya mashabiki kuanza kumzomea mshika kibendera huyo huku wengine wakimrushia makopo ya maji.
 Mashabiki wa Yanga wakishangilia....
 Mashabiki wa Etoile wanaodaiwa kuwa ni wa Simba wakifuatilia mtanange huo.....
 Ngassa akitulia Soka kifuani.....
 Kiungo mkabaji wa Etoile, Franck Kom, akipiga mpira mbele ya Amis Tambwe....
 Mrisho Ngassa (kulia) akijaribu kumramba chenga Franck Kom....
 Ngassa (kulia) akiwania mpira na beki wa Etoile....
 Beki wa Etoile, akimchezea rafu Ngassa.....baada ya kumshika
 Ngassa akiwa chini baada ya kuchezewa rafu, mwamuzi alipeta tukio hilo....
 Haruna Niyonzima, akishikwa na mchezaji wa Etoile.....
 Niyonzima, akifankiwa kiwatoka wachezaji wa Etoile....
 Simon Msuva, akimfinya beki wa Etoile....
Afande naye akiwa kazini kunasa matukio.....

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.