Habari za Punde

*UFUNGUZI WA MICHEZO YA VYUO VIKUU TANZANIA 2015 (NACTE INTER COLLEGE CHAMPIONSHIPS)

 Katibu msaidizi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (NACTE) Mhe. Alex Mkondola akikagua timu za Bandari na IFM wakati wa mchezo wa Ufunguzi kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwishoni mwa juma.
Katibu msaidizi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (NACTE) Mhe. Alex Mkondola  katikati akifafanua jambo wakati wa mchezo wa Ufunguzi kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwishoni mwa juma.
**********************************************
Na: Faraja Nyota, Dar
Fainali za kwanza za michezo ya vyuo vya elimu ya kati NACTE TANZANIA, zimezinduliwa siku ya jumamosi tarehe 18 kwenye viwanja vya chuo kikuu cha Dar es Salaam, ambapo Mgeni Rasmi aliyefanya Uzinduzi huo ni Katibu msaidizi wa NACTE, Mhe. Alex Mkondola.

Ufunguzi huo ulizihusisha timu zilizokuwa kundi A, pamoja na zile za kundi B zilizopo kwenye viwanja vya Chuo cha Mwalimu Nyerere Memorial-Kigamboni, katika mchezo wa mpira wa miguu uwenye msisimko mkubwa ukilinganisha na michezo mingine.

akizungumza wakati wa Uzinduzi huo Mgeni rasmi aliwaasa washiriki wote kuitumia michezo hii kama sehemu ya wao kubadilishana mawazo pamoja na kuijenga miili yao kimichezo " jambo hili la uwepo wa hii michezo ni jambo la kujivunia kutokana na kwambsasa wale wote wenye vipaji mtaviendeleza lakini kubwa ikiwa ni kubadilishana mawazo miongoni mwenu, isipokuwa natarajia kwamba mtaitumia michezo hii kushiiki kwa utulivu ili iweze kuleta tija na iwe ya msisimko kila mwaka" alisema Mkondola

Michezo hiyo inahusisha juma ya vyuo 18 vilivyofanikiwa kuingia hatua hiyo baada ya kufuzu kuvuka katika hatua ya awali ya makundi 11 yaliyokuwa na timu 10 kila kundi katika idadi ya vyuo 115 vya Dar es salaam na Pwani.

Fainali ya Michuano hiyo inatazamiwa kufanyika june 21 kwenye viwanjia vya chuo kikuu cha Dar es Salaam UDSM ambapo timu zilizopo kwenye michuano hiyo ni pamoja na  kundi A lenye timu za Mwalimu Nyerere Memorial Academy
Bandari College, College of Social Science, National Institute of Transport, Institute of Finance Management
Kilimanjaro Institute College.

timu zinazounda kunda B ni pamoja na St. Joseph College, College of Business Education, Elimu ya Watu Wazima,  Tanzania Institute of Accountancy (TIA) Muhimbili Medical Schools, College of Engineering and Technology huku kundi a mwisho likiwa na timu za Njuweni Institute of Hotel, Catering & Tourism Management, Tanzania Revenue Authority 
University of Dar es Salaam Business School, Bagamoyo College of Arts (TaSUBa), Dar es salaam City College(DACICO), Dar es Salaam Institute of Tecknology (DIT)

Wadhamini wa michezo hii ni pamoja na Pepsi, Vodacom, Equity Benk, CXC Tours & Safari, Clouds Media Group, Zinduka, Njuweni Institue & Cataring Menegement, Mlonge by Makai, DACICO, Mliman Radio na TV, TV 1, Tanzania Daima, Kikiz Productions, Events World, Global Publishers, Miss Demokrasia Tanzania, Michuzi Media Group na Mhe. Maxmillian Madoro.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.