Habari za Punde

*UZINDUZI WA KITABU CHA KUJIFUNZA KILINGALA CHA TSHIMANGA KALALA ASSOSA NA KAVASHA CLUB


Jumapili ya wiki hii Mei 03-2015, mwanamuziki mkongwe Tshimanga Kalala Assosa, anatarajia kuzindua kitabu kilichokuwa kikisubiriwa na wengi kwa muda mrefu cha "Jifunze LINGALA kwa Kiswahili".


Uzinduzi huo utaambatana na tukio kubwa la wana Dar Kavasha Club pamoja na chakula cha jioni cha pamoja (dinner) ambalo litafanyika ndani ya Ukumbi wa MRC inapofanyika shoo ya Club Raha Leo Show, kuanzia majira ya saa 12 jioni hadi saa 3 usiku. 

Aidha mwanamuziki huyo Tshimanga Kalala Assosa, amewahi pia kufanya kazi na bendi nyingi kubwa za hapa Afrika kama Negros-Success (akiwa na Bolhen na Bavon Marie), Orchestre Lipua Lipua, Orchestre Les Kamale,  (akiwa na Nyboma, Mulembu na Kizunga) pamoja na Fukafuka zote za Congo DRC. Kwa hapa Tanzania amefanya Mlimani Park Orchestra, Marquis Original, Orchestre Makassy, Orchestre Mambo Bado, Legho Stars na Bana Maquis, hivyo atapata fursa ya kukumbushia za kale ni dhahabu.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajia kutangazwa hapoa baadaye, wote mnakaribishwa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.