Mkurugenzi Mtendaji wa Tausi Dreams Foundation
Tausi Likokola na akisalimiana na baadhi ya wahitimu wa kidato cha sita mwishoni
mwa wiki wakati alipokuwa mgeni rasmi katika wa mahafali hayo shuleni Jangwani sekondari
iliyopo manispaa ya Ilala Jijini Dare s salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tausi Dreams Foundation
Tausi Likokola (wa pili kushoto) na baadhi wa viongozi wa shule wakielekea eneo la
mahafali ya kidato cha sita ya shule ya sekondari Jangwani yalifanyika mwishoni
mwa wiki ambapo Mkurgenzi huyo alikuwa mgeni rasmi. Wa kwanza kushoto ni Mkuu
wa Shule ya sekondari Jangwani Geraldine Mwanisenga.
Baadhi ya wahitimu wa kidato cha sita mwaka huu
wa Shule ya sekondari Jangwani wakielekea eneo la mahafali yao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tausi
Dreams Foundation Tausi Likokola akitoa hotuba yake wakati wa mahafali ya
kidato cha sita shule ya sekondari Jangwani mwishoni mwa wiki na kuwaasa
watumie nidhamu bora ambayo itawasaidia kufikia malengo yao waliyojiwekea
maishani mwao. Kushoto ni Mkuu wa Shule ya sekondari Jangwani Geraldine
Mwanisenga.
Mwanafunzi aliyepata vyeti mbalimbali vya
taaluma takribani saba kwa kufanya vizuri katika masomo ya Kemia, Biyolojia,
Fizikia, Hesabu, cheti cha kuwa mwanafunzi bora katika masomo, uongozi, uongozi
bora pamoja na zawadi Rosemary Mushi akipongezwa na Mgeni Rasmi na Mkurugenzi
Mtendaji wa Tausi Dreams Foundation Tausi Likokola na kukabidhiwa vyeti vyake
wakati wa mahafali ya kidato cha sita yalifanyika shule ya sekondari Jangwani mwishoni
mwa wiki.
Baadhi ya wahitimu wa
kidato cha sita mwaka huu wa Shule ya sekondari Jangwani wakimsikiliza Mgeni
Rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Tausi Dreams Foundation Tausi Likokola wakati wa
mahafali yao shuleni hapo mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wanafunzi wakitoa burudani wakati wa mahafali hayo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Barnaba Boy, akitoa burudani wakati wa mahafali hayo.
Wasanii wakitoa burudani .....
Kikundi cha wanafunzi
wa shule ya sekondari Jangwani wakionesha ukakamavu wao huku mmoja wao alyekuwa
juu ya wenzake akimakabidhi MC mic kwa ujasiri.
*********************************************
Na Eleuteri Mangi, Dar
Wanafunzi wa shule ya
sekondari ya Jangwani wameaswa kutumia muda wao vema wakiwa shuleni kwa kuwekeza
kwenye elimu ambayo inasaidia kumbadilisha mtu na hatimaye kubadilisha jamii
nzima.
Kauli hiyo imetolewa
mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi Mtendaji wa Tausi Dreams Foundation Tausi
Likokola alipokuwa mgeni rasmi wakati wa mahafali ya wanafunzi wa kidato cha
sita katika shule ya sekondari Jangwani iliyopo manispaa ya Ilala Jijini Dare s
salaam.
“Ukizaliwa mwanamke,
tambua kuwa wewe ni kiongozi wa kwanza katika jamii, hivyo tumia vipaji vyako
kama ulivyojaliwa na Mwenyezi Mungu ukizingatia suala la nidhamu ambayo ndiyo
msingi wa mafanikio yote yatakayowasaidia katika maisha yenu ndani ya jamii”
alisema Tausi.
Tausi alisisitiza kuwa
watu wengi duniani wanaofanikiwa wanaongozwa na nidhamu bora waliyonayo ambayo
imewasaidia kufikia malengo yao waliyojiwekea, wanafunzi hao wametakiwa kuiga
mfano huo ili waweze kufanikiwa maisha yao kwa manufaa yao binafsi, jamii na
taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkuu wa
Shule ya sekondari Jangwani Geraldine Mwanisenga alipokuwa akitoa taarifa fupi
ya shule kwa mgeni rasmi wakati wa mahafali hayo alisema kuwa shule yake ni
miongoni mwa shule kongwe nchini ambazo zinazofanya vizuri kitaaluma na masuala
mengine yasiyo ya kitaaluma.
Kuhusu taaluma, Mkuu
huyo alisema kuwa shule yake imeendelea kufanya vizuri na kushika nafasi ya juu
katika matokeo ya mitihani ya taifa ambapo mwaka huu imeshika nafasi ya kwanza
kwenye matokeo ya kidato cha nne miongoni mwa shule za sekondari za serikali
katika Mkoa wa Dar es salaam.
Mkuu huyo wa shule
alisema kuwa siri kubwa ya mafanikio yao inatokana na kujiweka malengo,
mikakati na kuhakikisha vyote inatekelezwa kwa wakati.
Miongoni mwa mikakati
hiyo ni kufundisha masomo ya ziada na rekebishi, kutoa motisha kwa walimu na
wanafunzi wanaofanya vizuri katika masomo, ushirikiano baina ya Bodi ya shule,
wazazi, wafanyakazi wanafunzi na wadau wengine wa elimu ikiwa ni chachu ya
mafanikio ya shule.
Aidha, Mkuu wa shule
mwalimu Geraldine amewaasa wahitimu hao watumie elimu waliyoipata wakiwa
shuleni hapo kama silaha ya ukombozi kwenye jamii, maana jamii inahitaji wasomi
ili kuikomboa kifikra, kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Naye mwanafunzi
aliyepata vyeti mbalimbali vya taaluma takribani saba kwa kufanya vizuri katika
masomo ya Kemia, Biyolojia, Fizikia, Hesabu, cheti cha kuwa mwanafunzi bora
katika masomo, uongozi, uongozi bora pamoja
na zawadi Rosemary Mushi alibainisha
kuwa ilikuwa ndoto yake kuja kuwa mwanafunzi bora maana alipokuwa kidato cha
nne zawadi hiyo ilienda kwa mwanafunzi mwingine ambapo hatua hiyo ilimpa hamasa
ya kusimamia azma yake kwa moyo wote.
“Leo ninafuraha sana
maana ilikuwa ndoto yangu kuja kuchukua vyeti vyote ambapo ilinilazimu kusoma
sana na kufaulu vizuri ili nifikie ndoto yangu ya maisha ya kuwa daktari wa
watoto” alisema Rosemary.
Rosemary aliushukuru
uongozi wa shule, walimu, wafanyakazi wasio walimu na wanafunzi wenzake kwa
ushirikiano mzuri alioupta kutoka kwao wakati wote alipohitaji masaada wao ili
kufikia malengo yake ya kufaulu vizuri masomo yake na kumuwezesha kusonga mbele
katika hatua nyingine ya elimu.
Shule ya sekondari
Jangwani ilinzishwa kwa historia ya kuwekwa jiwe la msingi liliwekwa mnamo Mei
28, mwaka 1928 na Kiongozi Mkuu wa ukoloni wa Mwingereza wakati huo Sir Donald
Cameroon na kuifanya shule hiyo kuwa na umri wa miaka 87 ambapo kwa sasa ina jumla
ya walimu 102, wafanyakazi wasi walimu 21, wanafunzi 1150 miongoni mwao
wanafunzi 70 ni wenye mahitaji maalum kulingana na mahitaji ya sera ya elimu
chini ya mataala wa elimu jumuishi uliohimiza kusomesha wanafunzi wenye
mahitaji maalum.









.jpg)
No comments:
Post a Comment