Habari za Punde

*YANGA YAWADUNDA 'WAPIGA DEBE' STAND UNITE MABAO 3-2

 Kiungo wa Yanga, Andey Coutihno, akichuana na beki wa Stand United, Pastori Athanas, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Yanga ilishinda mabao 3-2, yaliyofungwa na Amis Tambwe katika dakika ya 30, Mrisho Ngassa, dakika ya 45, na Simon Msuva, dakika ya 79 kwa mkwaju wa penati baada ya beki wa Stand kumwangusha Amis Tambwe katika eneo la hatari.

Mabao ya Stand United, yalifungwa na Kheri Khalifa, katika dakika ya 20 na 65.
 Mabeki wakichezeana undava, weka niweke.
 Mrisho Ngassa, akimtoka Haruna Chanongo.
Rajab Zahir akimdhibiti Chidiebele Abasalim. KWA MATUKIO YA PICHA ZA MTANANGE HUU ZITAWAJIA BAADAYE. KAA NASI

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.