Habari za Punde

*ABBAS MTEMVU ALIPOWATEMBELEA WAATHIRIKA WA MAFURIKO YOMBO

 Mtemvu akiitembelea Nyumba ya Bi Mwashamba Mwandoro maeneo ya Kurasini,  baada ya ukuta wa Nyumba kuanguka kutokana na Mvua zinazo endelea kunyesha Dar es Salaam.
 Mbunge wa Jimbo la Temeke na Mbunge wa Wabunge Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu (kulia) akiongozana na Meya wa Temeke Maabad Suleiman (katikati) na Naibu Meya wa Jimbo hilo Juma Mkenga  wakati wa ziara ya  kutembele walio athirika na Mvua zinazoendelea kunyesha
  Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtevu akiyapima maji kwa kuingia katika dimbwi lililokuwa limejaa maji na kushuka katika Gari alilokuwa amepanda na kumsaidia Dereva wa Gari  lenye usajili T 526 DDR lililonyuma ya Mbunge huyo .
  Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu akimsaidia kumuelekeza Dereva wa Gari T 526 DDR baada ya uonekana kusuasua.
 Maji ya Mvua yakiwa yamezingira Nyumba maeneo ya Wailesi Temeke
 Mjumbe wa Shina kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM)  Juma Salum  (wakwanza kishoto) akitoa maelezo kwa Mbunge wa Jimbo hilo mara alipofika kuwaona
Baadhi ya mitaa iliyoathirika na mvua hiyo.
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Abdon Kidege, akimweleza jambo Mbunge wa Jimbo hilo Abbas Mtemvu wakati wa ziara ya kuwatembelea wananchi waliopatwa na mafuriko ya Mvua zinazo endelea kunyesha.
 Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akizungumza na wananchi waliopatwa na mafuriko maeneo ya Wailesi.
 Madereva wa Magari ya Abiria yanayo fanya safari kati ya Tandika - Yombo Kilakala kupitia Daraja la Tazara na Tandika kwa Limboa wakishirikiana kujaza viroba vya mchanga na kuweka sehemu ya maeneo ya  Barabara hiyo ili waweze kupita kwa urahisi     
 Baadhi ya Madereva wakijitolea kujaza mchanga katika viroba ili kutengeneza njia magari yaweze kupita.
 Magari yakipita kwa shida na eneo hilo linauterezi.
 Baadhi ya magari yalilazimika kushushia abiria katikati ya Daraja.
  Zaidi ya wanafamilia 55 wayakimbia makazi yao katika maeneo ya Yombo Kilakala kwa Bongotonyo, kutokana na Nyumba zao kujaa maji.
 Mbunge Mtemvu akipima maji
 Mbunge Mtemvu akipima kina cha maji 
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Yombo Relini Yusufu Marko (kulia) akimweleza jambo, Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, wakati alipofika katika maeneo hayo baada ya kuzunguuka katika maeneo tofauti kukagua maeneo yaliyoathirika na mvua.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.