Habari za Punde

*MAYWEATHER AMCHAPA PACQUIAO KWA POINTI, MASHABIKI DAR WAKESHA WAKISUBIRIA PAMBANO LACHEZWA ASUBUHI

 Bondia Floyd Mayweather (kushoto) akimsukumia konde zito mpinzani wake, Manny Pacquiao katika raundi ya kwanza tu ya mchezo kati ya raundi 12 za pambano hilo. Pambano hilo lilimalizika kwa Maywether kushinda kwa Pointi. 

Pambano hilo lililokuwa likisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa pande zote mbili liliwatesa mashabiki wengi na hasa wa jijini Dar es Salaam, ambao wengi wao walikesha wakilisubiria kuanzia mida ya sita jana usiku wakati pambano hilo lilichezwa majira ya saa moja kasoro asubuhi.

Mashabiki wengi waliojazana katika Kiota cha Dagaa Dagaa pale maeneo ya Legho, Sinza jijini Dar es Salaam, walisikika wakilaani na kujilaumu kutokana na kukesha wakilisubiria hali ya kuwa walikuwa na uwezo wa kulala na kuamka asubuhi na kuliona.

Aidha baadhi ya mashabiki wa Manny Pacquiao, wengine walianguka na wengine kuondoka mahala hapo wakiangua vilio kutokana na bondia wao kupigwa huku wengine wakiwa na machungu zaidi kwa kupoteza pesa zao walizokuwa wamebeti baina yao na mashabiki wa Mayweather, yaani kuwekea na dau.

Kwa ushindi huo Maywether ameendeleza na kuvunja rekodi ya historia Bondia wa zamani Mohammed Ally, ya kutopigwa michezo 50
 Mwamuzi wa pambano hilo akiwaamulia na baada ya kengele kulia.
 Manny Pacquiao akimsukumia konde zito, Mayweather, lililotaka kumpeleka chini.
 Ilikuwa ni piga nikupige...
 Mabondia hao wakitambiana kabla ya pambano hilo kuanza....
 Mashabiki wa mabondia hao wakifuatilia pambano hilo katika kiota cha Dagaa Dagaa. Legho Sinza jijini Dar es Salaam.
  Mashabiki wa mabondia hao wakifuatilia pambano hilo katika kiota cha Dagaa Dagaa. Legho Sinza jijini Dar es Salaam.
  Mashabiki wa mabondia hao wakifuatilia pambano hilo katika kiota cha Dagaa Dagaa. Legho Sinza jijini Dar es Salaam.
Ndundi zikiendelea....

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.