Eneo zilipokuwepo nyumba za makazi ya askari polisi wa Kituo cha Oysterbay, zikiwa tayari zimebomolewa ili kupisha ujenzi wa Maduka ya Kisasa katika eneo hilo, 'Shopping Mors', ambapo pia tayari ujenzi wa Kituo kipya cha Polisi umeshaanza upande wa Ubalozi ili kubomolewa kile cha zamani ili kukamilisha ramani ya ujenzi huo unaotarajia kuanza karibuni.
Wadau wa karibu wa Mtandao huu walitonya kuwa eneo hilo tayari lilishauzwa kwa mwekezaji huyo aliyeanza kutekeleza ujenzi, na askari waliokuwa wakiishi kambini humo kupewa taarifa za kuhama na wengine kuhamia katika majengo yaliyojengwa na mwekezaji huyo huko eneo la Kijichi.
Aidha imeelezwa kuwa mpaka hivi sasa asilimia kubwa ya askari waliokuwa wakiishi kambini humo wameshahama na kubomolewa majengo yao, ambapo wamesalia baadhi tu, ambao nao watakapohama basi nyumba zote zitabomolewa.
Jengo linaloelezwa kuwa ndiyo Kituo cha Polisi kipya na Ofisi za Jeshi hilo, ikiwa katika hatua za mwisho mwisho kukamilika katika eneo hilo.
Eneo hilo likionekana la wazi baada ya zoezi la ubomoaji.
Nyumba zikiwa tayari zimebomolewa kiasi cha kuwa wazi na kuonekana hadi upande wa pili wa barabara ya Ali Hassan Mwinyi.
Nyumba zote chaliiiiii
Muonekano wa ofisi hiyo inayoendelea kujengwa.





No comments:
Post a Comment