Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MAREHEMU JOHN NYERERE DAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu John  Nyerere, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Msasani, jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2015. Marehemu John anatarajia kuzikwa keshokutwa nyumbani kwao Butiama.





 Marehemu John anatarajia kuzikwa keshokutwa nyumbani 

kwao Butiama. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu John Nyerere, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Msasani, jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maombolezo cha msiba wa marehemu John Nyerere, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Msasani, jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, wakatialipowasili nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Msasani jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu John Nyerere. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, wakati alipowasili nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Msasani jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu John Nyerere. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na baadhi ya viongozi na waombolezaji nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Msasani jijini Dar es Salaam, leo wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu John Nyerere.
Mama Tunu Pinda, pia akijumuika na waombolezaji.
Sehemu ya waombolezaji waliohudhulia ibada hiyo.
Waombolezaji
Mzee Joseph Warioba, akisikitika wakati akiwa kwenye msiba huo.
Mdogo wa marehemu akisoma wasifu wa marehemu.
Wazee wanapokutana, mzee Magula na mzee Slaa, wakifurahia jambo baada ya kukutana uso kwa uso.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.