Habari za Punde

*WAKAZI WA JANGWANI WAHAMIA STENDI YA MABASI YAENDAYO KASI

 Baadhi ya wakazi waishio Bonde la Jangwani jijini Dar es Salaam, wakiwa katika Stendi mpya ya Mabasi yaendayo kasi eneo la Jangwani baada ya kukimbia makazi yao yaliyokumbwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar na nchini kote. Wakazi hao wameweka kambi katika stendi hiyo na familia zao huku wanaume wakigeuka walinzi nyakati za usiku kwa kutolala ili kulinda mali zao na familia zao.
 Maisha yakiendelea.
 Barabara hiyo ya Jangwani kiwa imetapakaa uchafu utokanao na maji yaliyojaa na kupita juu ya barabara na kusababisha kufungwa kwa muda barabara hiyo, hivi majuzi.
Hivi sasa hali ni shwari kwani magari yanapita kama kawaida katika barabara hiyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.