Habari za Punde

*WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI AKUTANA NA WANANCHI WA TABORA.

  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi akisisitiza jambo wakati alipozungumza na Wakuu wa sekta mbalimbali mkoani Tabora leo kuhusiana na masuala yanayohusu sekta ya ardhi mkoani humo katika ukumbni wa mikutano wa Isike. Kulia ni mkuu wa Wilaya ya Tabora Mh Suleiman Kumchaya na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Bi Kudra Mwinyimvua.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi akizungumza na Wananchi wa Eneo la Malabi katika Manispaa ya Tabora, kuhusiana na mgogoro wa Ardhi unaowakabili wananchi hao ambao unaotokana na Manisapaa kutowalipa fidia ya maeneo yao.
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mh Suleiman Kumchaya akijadiliana jambo wakati Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvu alipotembelea eneo la Malabi katika Manispaa ya Tabora kusikiliza matatizo ya Ardhi yanayo wakabili wananchi wa eneo hilo leo. Picha/Clarence Nanyaro.
*****************************************************
Na Clarence Nanyaro - Wizara ya Ardhi, Tabora.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amewasili mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi ya siku tano. Mhe: Lukuvi amekutana na kuzungumza na Wakuu wa sekta mbalimbali wa mkoani huo kuhususiana na masuala ya ardhi.

Akiwa ameanza ziara yake akiwa ameongozana na viongozi wa mkoa huo akiwemo mkuu wa Wilaya ya Tabora Bw. Suleiman Kumchaya na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Bi Kudra, Mhe. William Lukuvi amepata fursa ya kuzungumza na kusikiliza hoja mbalimbali za Wananchi wa eneo la Malabi katika Manispaa ya Tabora.

Pamoja na mambo mengine wananchi hao wamemweleza mgogoro wa Ardhi unaowakabili ambao unaotokana na Manispaa hiyo kutowalipa fidia ya maeneo yao ambapo Mhe. Lukuvi ameahidi kulishughulikia suala hilo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.