Muhubiri Mkuu wa Sherehe za Makambi mtaa wa Manzese Mch. Idelphonce
Tirumanywa akihutubia watu waliohudhuria sherehe hizo. Ujumbe Mkuu
"Mtizame Yesu Ukaishi"
Kwaya Maalum ya Jangwani kutoka Shinyanga ikitumbuiza wakati wa Sherehe za
Makambi ya Mtaa wa Kanisa la Waadventista Wasabato Manzese.
Kikosi maalum cha vijana wadogo wa Kanisa la Waadventista Wasabato Manzese
(Wavumbuzi) wakitembea kwa mwendo wa gwaride kuelekea jukwaani kwa ajili ya
program maalum kwenye sherehe za makambi.
Watoto wa
Mtaa wa Manzese wakionesha program maalum jukwaani kwenye sherehe maalum za
makambi ya Manzese. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Mch. Amos Lutebekela (Kushoto) akimkabidhi zawadi ya shukrani mkufunzi wa
vijana Bw. Chris Buhatwa wakati wa kuhitimisha sherehe za Makambi mtaa wa
Manzese
Baaadhi ya washiriki wa sherehe za makambi wakisikiliza kwa makini vipindi vinavyoendelea kwenye Makambi ya Mtaa wa Manzese
Baadhi ya wabatizwa wakipokelewa na wachungaji na wazee wakanisa wakati wa kuhitimisha
sherehe za makambi.
Mch. Idelphonce Tirumanywa akinyoosha mkono juu kuomba wakati wa kufanya huduma maalum ya ubatizo kwa watu walioamua kujiunga na kanisa la waadventista wasabato ulimwenguni.
Kwaya ya Angaza ikimwimbia Mungu siku ya kuhitimisha sherehe za makambi
Manzese. Picha zote na Sarah Reuben
****************************************
Sherehe za Makambi kwa mwaka 2015 katika Mtaa wa Manzese zimemalizika kwa
kishindo cha kubatiza waumini ishirini na saba (27) ambao wameamua kumpokea
Yesu kwa kujiunga na kanisa la Waadventista Wasabato Manzese.
Akizungumza na waumini wa kanisa hilo wakati wa kuhitimisha sherehe hizo
mwishoni mwa wiki, Mchungaji Idelphonce Tirumanywa amesisitiza kuwa kanisa kuendelea kuwalea vyema waumini wapya waliojiunga na
kanisa hilo. Mch. Tirumanywa pia ameendelea kuwaasa waumini wote wa kanisa la
waadventista wasabato kuwa mfano bora kwa jamii kwa kuonesha matendo mema
yatakayo warudisha watoto wa Mungu waliopotea nyumbani.
“Ni wakati wakurudi nyumbani, dunia ipo kwenye hatari kubwa, tena kubwa
sana. Tunapoishukuru serikali yetu kwa uhuru wa kuabudu, waadventista wasabato
wote amkeni muumtangaze Mungu ili watoto wa Mungu waache dhambi na kurudi
nyumbani”, alisistiza Mch. Tirumanywa.
Sherehe za makambi ya mtaa wa Manzese yalihudumiwa na kwaya maalum kutoka
Sauti ya Jangwani Shinyanga wakishirikiana na kwaya tatu (3) zinazounda mtaa
huo yaani Angaza, Mbiu na Sauti ya Nyikani zote kutoka Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment