Uongozi wa kundi la TOT umepania kuwashusha jukwaani wasanii wa muziki wa Bongo Flava, wasiokuwa na nidhamu ya kazi katika kipindi cha kampeni 2015.
Akizungumza na mtandao huu Kiongozi wa Mipango na Uendeshaji wa kundi la TOT, Jarry Juma, alisema kuwa mwaka huu wamepania kuwanyima jukwaa na kuwashusha wasanii wote wa Bongo Flava watakao kiuka taratibu za kazi katika kipindi cha Kampeni za CCM.

Aidha alisema kuwa wasanii wengi wa muziki wa kizazi kipya 'Bongo Flava', mara nyingi wamekuwa wakijiona kama nao ni 'Ma VIP' kutokana na kwamba wamekuwa wakiharibu taratibu za kazi na kuvunja ratiba kwa kufika muda ule wakati anawasili Mheshimiwa Rais au Mgombea na kuvamia jukwaa.
''Wasanii wengi wanakuwa tayari wameshapewa ratiba lakini kwa kujiona na waoa ni Baab kubwa na wao wanachelewa kufika eneo la tukio na kusubiri dakika za mwisho ili wakute TOT imeshawajazia watu wao wafike na kuimba tu jukwaani.

Safari hii tumepanga hatutakubaliana na utaratibu huo, kama tumepewa ratiba ya kupiga nyimbo mbili TOT na nyimbo mbili Wasanii wa Bongo Flava basi iwe hivyo hivyo na kama wameambiwa muda wa kufika eneo la tukio ni saa mbili asubuhi na wafanye hivyo, vinginevyo wakichelewa halafu wanakuja wakati kiongozi anaingia kwenye mkutano, hatutawaruhusu kupanda jukwaa letu wala kuwaruhusu kutumia vyombo vyetu,ili wajifunze taratibu za kazi au waje na vyombo vyao'',alisema Jerry Juma.

No comments:
Post a Comment