Habari za Punde

*UZINDUZI WA BABARA KASKAZINI PEMBA

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikata utepe kufungua Barabara ya Wete- Gando na Wete-Konde katika Mkoa wa Kaskazini Pemba  katika ziara ya kuzindua miradi ya maendeleo katika Mkoa huo,(kushoto) Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Issa Haji Ussi.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Issa Haji Ussi (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk.Juma Malik Akili (wa pili kushoto) na Waziri wa Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban wakitembea katika  Barabara ya Wete-Gando baada ya kuizinduliwa rasmi juzi,katika katika ziara ya kuzindua miradi ya maendeleo Mkoa wa Kaskazini Pemba.
 Baadhi ya Viongozi na Wafanyakazi wa Wizara ya Mindombinu na Mawasiliano wakiwa katika sherehe ya uzinduzi wa Barabara ya Wete-Gando,Wete-Konde Mkoa wa Kaskazini Pemba uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,sherehe zilizofanyika viwanja kijiji cha Ukunjwi.
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Ukunjwi na Viongozi wakiwa katika sherehe za uzinduzi wa Barabara ya Wete-Gando,Wete-Konde zilizofanyika kijijini hapo Barabara iliyozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein juzi katika ziara ya kuzindua miradi mbali mbali ya Maendeleo katika Mkoa wa Kaskazini Pemba. Picha na Ikulu

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.