Nahodha wa timu ya Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro', (katikati) akishangilia na wachezaji wenzake huku akiwa na Ngao ya Hisani baada ya kukabidhiwa na Kamanda Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (nyuma yake) baada ya kuibuka kidedea katika mchezo wa Ngao ya Hisani kati yao na Azam Fc,mchezo uliomalizika bila kufungana katika muda wa dakika 90,na kupigiana penati tano tano huku kila timu ikikosa penati moja na kufikia kupiga penati moja moja.
Katika hatua hiyo Ame Zungu, alikosa huku Kelvin Yondani, akiwainua mashabiki wake kwa kupiga penati ya mwisho na kuibua kidedea. Waliokosa penati katika hatua ya awali, alikuwa ni Nadir Haroub kwa upande wa Yanga na Pascal Wawa kwa upande wa Azam Fc.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia ushindi....
Kutoka (kushoto) ni Malimi Busungu, Godfrey Mwashiuya na Deus Kaseke, wakishangilia ushindi....Raha ya mechi Bao.....KWA MATUKIO ZAIDI YA PICHA ZA MTANANGE HUU KAA NASI HAPO BAADAYE.



No comments:
Post a Comment