Wakimbizi kutoka nchini Burundi
walio katika kambi ya Nyarugusu wakiwa wamebeba Viroba vya Unga wa Mahindi jana,
muda mfupi baada ya kugawiwa chakula hicho na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia chakula
(WFP), lililoweka kituo chake katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu wilayani Kasulu,
mkoani Kigoma.
Byesige Josephat (anaye mimina mafuta) na Hezron Mtangirwa (kushoto), wakimbizi kutoka Burundi waliohifadhiwa kambi ya Nyarugusu wakipima mafuta ili waweze kuyagawa kwa wakimbizi wenzao jana,
Kinamama wakimbizi toka Burundi wakipata mgao wao wa unga
Mkimbizi Irene Ntibelenda (katikati) akiwa pamoja na ndugu yake Sengiyu Mvajeme (kulia) baada ya kupokea mgao wa chakula
Josef Ntukugurya akifunga Viroba vya unga wa mahindi jana baada ya kupokea mgao
Sehemu ya shehena ya chakula. PICHA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI –
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment