Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius
Likwelile wa kwanza kulia akiendelea kufanya majadiliano na ujumbe wa JICA ukiongozwa
na Rais wa JICA Bw. Hiroshi Kato wa pili
kulia.
Ujumbe
wa Tanzania na Ujumbe wa JICA wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr.
Servacius Likwelile wakati wa majadiliano ya kuwekeza katika sekta ya umeme,
utalii na kuboresha mazingira ya biashara.
*****************************************
Serikali
ya Jumhuri ya Muungano wa Tanzania yapata dola milioni 280 kutoka Benki ya
Dunia na Japani, fedha hizo zitatumika kusaidia mipango mbalimbali nchini
Tanzania.
Akiongea na Makamu wa Rais wa
Benki ya Dunia ukanda wa Afrika Bw. Makhtar Diop na Rais wa Shirika la
Maendeleo ya Japan-JICA Bw. Hiroshi Kuto, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius
Likwelile alisema dola milioni 230 zimetolewa na Benki ya Dunia. Kiasi
cha Dola milioni 100 ni kwa ajili ya
kuhimiza mambo ya uwazi katika utawala, dola milioni 80 ni kwa ajili ya
kuboresha mazingira ya kufanya biashara na dola milioni 50 ni kwa ajili ya
kuboresha sekta ya hifadhi ya jamii yaani
pensheni.
Shirika
la Maendeleo la Japan (JICA) wamethibitisha kuendelea kuunga mkono Serikali ya Tanzania katika mipango ya maendeleo. Wakiwa katika
kikao na ujumbe kutoka Tanzania, Bw. Hiroshi Kato ambaye ni Makamu wa Rais wa
shirika hilo alisema kuwa , Serikali ya
Japan kupitia shirika lao la maendeleo ( JICA) lina mipango ya kuunga mkono
Tanzania na Kenya watajenga barabara
ambayo itaunganisha Arusha na Mombasa
kwa kiwango cha juu ili kuweza kurahisisha mazingira ya biashara na utalii. Bw.
Kato katika mazungumzo yake aliongeza kuwa bado wao wako tayari kusaidia
kupitia bajeti kuu ya Serikali kama vile ambavyo wamekuwa wakifanya miaka ya
nyuma.
Akifafanua
kuhusiana na sekta ya hifadhi ya jamii Dkt. Likwelile alisema kuwa uboreshaji
wa pension umeahirishwa kwa sasa na wameomba Shirika la kazi la Kimataifa (ILO)
wafanye mapitio ya sekta hiyo na baada ya mapitio hayo ndio tutajua ni masuala
gani tunaweza kuyazingatia ili kuboresha sekta yetu ya hifadhi ya jamii.
Katika
majadiliano na viongozi wa benki ya Dunia Dkt. Lilkwelile aliwaeleza kuwa, Tanzania kuna
changamoto kubwa kwasababu uzalishaji wa umeme kupitia maji umepungua kutokana
na kina cha maji kupungua katika maeneo ya uzalishaji hivyo tunategemea gesi.
“Tunategemea
gesi ya Kinyerezi One ambayo inatupatia megawatts 405-407, na vilevile tunapata
umeme kutokana na matumizi ya mafuta ambapo ni gharama kubwa na uzalishaji
haujafikia lengo ambalo ni mahitaji yetu ya siku ambayo tunapata. Tuna
mapungufu ya megawatts160, suala hili limeleta shida sana kwenye bajeti yetu”. Alisisitiza Likwelile
Benki
ya Dunia watashirikiana na Idara ya Serikali ya Uingereza ya maendeleo ya
Kimataifa (DFID) pamoja na Japan kuwekeza katika reli ya kati ili kuunga mkono
jitihada zetu za kuboresha huduma ya reli nchini Tanzania, Likwelile aliendelea
kufafanua.
Kwa
upande wa maendeleo ya uchumi wa Tanzania ni kwamba uchumi bado unakuwa kati ya
asilimia 6.5 mpaka 7, mfumuko wa bei umeshuka japokuwa unapanda kidogo kufikia
asilimia 6.4, akiba ya fedha za kigeni bado inawezesha Tanzania kuingiza bidhaa
za karibu miezi minne, aliongeza Dkt. Likwelile.
Katika
majadiliano hayo Rais wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Bw. Diop alisisitiza
kuwa Tanzania iweke msisitizo mkubwa kwenye kilimo chenye tija na cha
kibiashara pamoja na kuwekeza kwenye
miundombinu ambayo itasaidia uchumi kuimarika hasa kwenye nishati, reli,
barabara, mawasiliano pamoja na kuwekeza kwa vijana kwani ni wengi sana na wanahitaji uhakika wa kupata ajira. Tukiweza
kufanya kilimo kikawa cha tija na kuwekeza kwenye viwanda vidogovidogo na
kuwapa vijana elimu ambayo itawasaidia kuweza kujitegemea, Tanzania itaweza
kusonga mbela.
Akiendelea
kufafanua Bw. Diop alisema, kutokana na uchumi wa Tanzania ulivyo hakuna sababu
ya kukusanya mapato yetu ya kodi kwa kiwango cha sasa, tuna uwezo wa kwenda
hadi asilimia 12 ya pato la Taifa. Naye Dkt. Likwelile alimuhakikishia Rais wa
Benki ya Dunia kanda ya Afrika Bw. Diop kuwa lengo la Tanzania ni hili ila
tunahitaji uwekezaji ili tuweze kufikia lengo tuulilokusudia, maana tumeweka ukomo wa fedha angalau tufikie
mpaka asilimia14.5 lakini tunaweza kwenda mpaka asilimia 17 – 20 katika miaka
mitatu ijayo.
Katika
kuhitimisha majadiliano hayo Dkt. Likwelile alisema kwamba ushirikiano kati ya
Tanzania na Benki ya Dunia ni mzuri na mkubwa sana. Kiwango cha fedha ambacho
tunakipata kutoka kwao kinazidi kuongezeka na wameweza kuturuhusu kuwekeza
kutumia mlango mwingine mfano kwenye Chama
cha Maendeleo ya Kimataifa(IDA) na pia kwa sasa tumeweza kupata fedha kupitia Benki
ya Kimataifa ya ujenzi na maendeleo(IBRD) kwa ajili ya upanuzi wa Uwanja wa
Ndege wa Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment