Habari zilizotufikia muda mchache uliopita zinasema kuwa, Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila (pichani juu) amefariki dunia katika ajali ya gari binafsi alfajiri ya leo eneo la Msolwa-Chalinze, wakati akitokea mkoani Morogoro akirejea jijini Dar es Salaam, akiwa na wenzake watatu, ambao ni majeruhi. Mwili wa marehemu umepelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Tumbi. Picha ya gari alilopata nalo ajali (chini ya picha yake)
Mtandao huu wa Sufianimafoto blog unaungana na wanachama wa DP pamoja na watanzania wote kwa jumla katika kuomboleza kifo cha Mchungaji Mtikila, Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Mchungaji Mtikila Amen.


No comments:
Post a Comment