Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha DP Marehemu Mchungaji Christopher Mtikila, wakati wa kuaga mwili leo Oct 07, 2015 katika ukumbi wa Karimjee jiji Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wananchi, ndugu, Jamaa na marafiki wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha DP Marehemu Mchungaji Christopher Mtikila, wakati akitoa salamu za rambirambi katika shughuli ya kuaga mwili leo katika ukumbi wa Karimjee jiji Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji ndugu, jamaa na wanachama wa UDP baada ya kutoa heshima za mwisho marehemu Mchungaji Christopher Mtikila, leo katika ukumbi wa Karimjee jiji Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment