Na Miraji Msala, Dar
MWANASOKA
wa Kimataifa wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta, ametinga katika kinyang’anyiro cha tuzo za kimsaka
mwanasoka Bora wa Mwaka wa Afrika.
Samatta, ameingia katika
kinyang'anyiro hicho akichuana na mwanasoka mahiri wa Ivory Coast, Yaya Toure,
huku Samatta, akiwania tuzo hiyo kwa mwanasoka anayecheza Soka ndani ya Afrika.
Na Yaya Tpure akiingia
kuwania Tuzo hiyo kwa mwanasoka bora wa Afrika anayecheza nje ya Afrika.
Taarifa
ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa imetoa orodha zote mbili za Mwanasoka
Bora wa Mwaka Afrika na Mwanasoka Bora wa Mwaka Anayecheza Afrika.
Katika
tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka Anayecheza Afrika, Samaatta mwenye umri wa
miaka 23 anayekipiga katika timu ya TP Mazembe ya DRC, anachuana na Abdeladim
Khadrouf wa Moghreb Tetouan ya nyumbani, Morocco, Abdelmalek Ziaya wa ES SETIF
ya nyumbani, Algeria, Ahmed Akaichi wa Esperance ya nyumbani, Tunisa,
Andiramahitsinoro Carolus wa Madagascar anayechezea USMA ya Algeria na Baghdad
Bounedjah wa Algeria anayechezea Etoile du Sahel ya Tunisia.
Wengine ni Bakri el Madina wa
El Merriekh ya nyumbani, Sudan, Bassem Morsi wa Zamalek ya nyumbani, Misri,
Boris Moubhio wa AC. Leopards ya nyumbani, Kongo-Brazzaville, Djigui Diarra wa
Stade Malien ya nyumbani, Mali na Felipe Ovono wa Guinea anayechezea Orlando
Pirates ya Afrika Kusini.
Wamo
pia Guelassiognon Sylvain Gbohouo wa Ivory Coast anayecheza na Samatta T.P
Mazembe, Hazem Emam wa Zamalek ya nyumbani, Misri, Hocine Ragued wa Esperance
ya nyumnbani, Tunisia, Kermit Erasmus wa Orlando Pirates ya nyumbani Afrika
Kusini na Malick Evouna wa Gabon, anayechezea Al Ahly ya Misri. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Wamo
pia Mohamed Koffi wa Burkina Faso anayechezea Zamalek ya Misri, Mohamed Meftah
wa USMA ya nyumbani, Algeria, Moudather el Tahir wa El Hilal ya nyumbani,
Sudan, Oupa Manyisa wa Orlando Pirates ya nyumbani Afrika Kusini, Robert
Kidiaba wa T.P Mazembe ya nyumbani, DRC, Roger Assale wa Ivory Coast
anayechezea T.P Mazembe, Thamsanqa Gabuza wa Orlando Pirates ya nyumbani Afrika
Kusini na
Zein
Edin Farahat wa USMA ya nyumbani, Algeria.
Katika
tuzo Ya Mwanasoka Bora wa Mwaka Afrika, Yaya Toure wa Ivory Coast na Manchester
City ataitetea dhidi ya Ahmed Musa wa CSKA Moscow ya Urusi na Nigeria, Andre
Ayew wa Swansea City ya England na Ghana, Aymen Abdennour wa FC Valence ya
Hispania na Tunisia, Baghdad Bonjah wa Etoile du Sahel ya Tunisia na Algeria.
Wengine
ni Bassem Morsi wa Zamalek ya Misri, Chrisitian Atsu wa Bournemouth ya England
na Ghana, Dieu Merci Mbokani wa Norwich ya England na DRC, El Arbi Hillel
Soudani wa Dynamo Zagreb ya Croatia na Algeria, Faouzi Ghoulam wa Napoli ya
Italia na Algeria na Ferebory Dore wa Angers ya Ufaransa na Kongo.
Wamo pia Gervais Yao Kouassi
wa Rome ya Italia na Ivory Coast, Ibrahima Traore wa Borussia Monchengladbach
ya Ujerumani na Guinea, Javier Balboa wa Al-Faisaly ya Saudi Arabia na
Equatorial Guinea, Heldon Ramos wa Rio Ave ya Ureno na Cape Verde, Mame Diouf
wa Stoke City ya England na Senegal.
Wamo
pia Max Alain Gradel wa Bournemouth ya England na Ivory Coast, Mehdi Benatia wa
Bayern Munich ya Ujerumani na Morocco, Modather Al Tayeb “Karika” wa El Hilal
ya Sudan, Mohamed Salah wa AS Roma ya Italia na Misri, Nicolas Nkoulou wa
Marseille ya Ufaransa na Cameroon na Pierre-Emerick Aubameyang wa Borussia
Dortmund ya Ujerumani na Gabon.
Wengine
ni Robert Kidiaba wa T.P Mazembe,
Rudy
Gestede wa Aston Villa ya England na Benin, Riyad Mahrez wa Leicester City ya
England na Algeria, Sadio Mane wa Southampton ya England na Senegal, Serge
Aurier wa Paris Saint Germain ya Ufaransa na Ivory Coast na Seydou Keita wa
Rome ya Italia na Mali.
Wengine
ni Sofiane Feghouli wa Valencia ya Hispania na Algeria, Stephane Mbia wa
Trabzonspor ya Uturuki na Cameroon, Thievy Bifouma wa Granada ya Hispania na
Kongo, Victor Wanyama wa Southampton ya England na Kenya na Vincent Aboubakar
wa Porto ya Ureno na Cameroon.
Wengine
ni Vincent Enyeama wa Lille ya Ufaransa na Nigeria, Yacine Brahimi wa Porto ya
Ureno na Algeria, Yannick Bolasie wa Crystal Palace ya England na DRC na Yasine
Chikhaoui wa Al-Gharafa ya Qatar na Tunisia.


No comments:
Post a Comment