Habari za Punde

*MKUTANO WA TUME NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA, ZATOLEWA SIKU NANE KUHAKIKI TAARIFA KITUO CHA KUPIGIA KURA

Na Anitha Jonas-Maelezo, Dar es salaam
Tume ya Taifa ya Uchaguzi  yawaasa  wapiga kura kote nchini kuhakiki taarifa zao katika vituo vya vya kupiga kura siku nane kabla ya uchaguzi.

Hayo yamesema jana  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva alipokuwa akizungumza katika mkutano na viongozi wa vyama vya siasa uliyofanyika leo jijini Dar es Salaam,
Jaji Lubuva amesema kuwa lengo la mkutano huo ni  kushauriana na vyama vya siasa katika kuelekea siku ya uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba 25 mw`aka huu.

“Tume imepanga kuhakikisha kila mpiga kura mwenye sifa ya kupiga kura  anapata haki ya kupiga  kura na imeagiza wasimamizi wa kura kutoa nafasi za upendeleo kwa watu wenye ulemavu  wa aina mbalimbalina na imeandaa karatasi maalum za kupigia kura kwa watu wenye walemavu wa kuona”,alisema Jaji Lubuva.
Aidha Jaji Lubuva aliwasihii viongozi hao kunadi sera zao majukwaani badala ya kuilalamikia Tume katika majukwaa  wakati wa kampeni  pia amewasaa wanasiasa hao  kupeleka malalamiko yao katika ofisi husika na kuacha kukimbilia waandishi wa habari.
Mbali na hayo Mwenyekiti wa Tume hiyo aliendelea kusisitiza juu ya viongozi wa vyama vya siasa wanao walazimisha wapigia kura kubaki katika vituo vya kupigia kura kuacha kauli hizo kwani kwa uzoefu unaonyesha kwamba wafuasi wa vyama wanapokutana pamoja huweza kuchangia uvunjifu wa amani.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw.Kailima Ramadhani alisema Tume ilibani kuwa jumla ya watu 3,870 walioandikishwa hawakuwa raia wa Tanzania na hivyo vitambulisho vyao vimerejeshwa Tume na taarifa zao kufutwa kwenye kanzidata ya daftari la kudumu la kupiga kura.

Mpaka sasa tume imeshasambaza vifaa mbalimbali vya uchaguzi nchini, vifaa ambavyo havijasambazwa ni pamoja na karatasi za kura, wino maalumu, karatasi za matokeo na muhuri wa kituo kutokana na umuhimu wake ila vinatarajiwa kuisambazwa hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.