Habari za Punde

*RAIS MTARAJIWA DKT. MAGUFULI AKABIDHIWA CHETI CHAKE CHA USHINDI LEO, JIJINI DAR

 Rais Mteule wa awamu ya tano, Dk. John Magufuli akiyonyesha hati ya ushindi wa Urais, baada ya kukabidhiwa leo na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva, katika hafla ya kukabidhi hati hiyo iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Dk. Magufuli amekabidhiwa cheti hicho kufuatia kuibuka mshindi wa kiti cha Urais katika matokeo yaliyotangazwa na NEC, jana, ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu. Kushoto ni Makamu wa Rais Mteule, Mama Samia Suluhu Hassan.
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva akimkabidhi hati ya Ushindi Makamu wa Rais Mteule, Mama Samia Suluhu Hassan, katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Dk. John Magufuli
  Mama Samia akionyesha hati baada ya kukabidhiwa
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu, Damian Lubuva akiwapongeza Rais Mteule Dk. Magufuli, na Makamu wake Mteule. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

Rais Mteule wa Tanzania, Dk. John Magufuli akipongezana na Makamu wake pia Mteule, Mama Samia Suluhu Hassan, baada ya kukabidhiwa hati zao za ushini na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Msaafu Damaian Lubuva, leo Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam
 Rais Mteule wa Tanzania, Dk. John Magufuli akimuonyesha hati ya ushindi, aliyekuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Anna Mghwira, baada ya kukabidhiwa hati hiyo na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam
 Rais Jakaya Kikwete akimpongeza Rais Mteule, Dk. John Magufuli, baada ya kukabidhiwa hati ya ushindi wa kiti cha Urais
 Dk. Magufuli akimpa akishike cheti hicho Rais Jakaya Kikwete
 'Sasa ni huyu" Rais Kikwete akichombeza wakati alipoonyeshwa cheti cha ushindi wa Urais na Dk. Magufuli
 Rais Mteule Dk. Magufuli akimpongezwa na Mkewe Mama Jannet Magufuli, baada ya kukabidhiwa hati ya ushindi wa Urais. Kushoto ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete. na kulia ni Makamu wa Rais Mteule  Mama Samia Suluhu Hassan
 Dk. Magufuli akipongezwa na Dk. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Katikati yao ni Rais Jakaya Kikwete na Kushoto ni Spika wa Bunge Anna Makinda
 Mama Samia akipongezwa na Mama Salma Kikwete. Kushoto ni Rais Kikwete
  Dk. Magufuli akipongzwa na Makamu Mwenyekiti mstaafu, wa CCM, Pius Msekwa. Katikati yao ni Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi
 Rais Mteule wa Tanzania, Dk. John Magufuli akipongezwa na Rais Mstaafu wa Nigeria Goodluck Jonathan, baada ya kukabidhiwa hati
 Dk. Magufuli akionyesha hati yake kwa wananchi baada ya kukabidhiwa hati hiyo
 Wadau wakiwa ukimbini
 Makamu wa Rais Mteule, Mama Samia akiwapungia wananchi mkono baada ya kupewa hati yake
 Mama samaia akiwasalimia wananchi ukumbini baada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi
 Aliyekuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya ACT, Anna Mghwira akimpongeza Dk. Magufuli, kwa ushindi aliopata
Picha ya pamoja
 Picha ya pamoja
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimpongeza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva  baada ya kukabidhi cheti cha Usnhindi wa Urais kwa Dk. Magufuli. Wapili ni Rais Kikwete na kulia ni Mama Samia
 Picha ya pamoja, Dk. Magufuli, Rais Kikwete, Mama samia na Jaji Mstaafu Lubuva
 Picha ya pamoja
 Rais wa Zamani wa Naigeria Goodluck Jonathan akiwa katika picha ya pamoja na Dk. Magufuli,  Rais Jakaya Kikwete, Mama Samia na Spika wa Bunge Anna Makinda
 Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akimpongeza Dk. Magufuli
 Picha ya Pamoja, Dk. Magufuli na Viongozi wa dini waliohudhuria
 Mwenyekiti wa IPP Reginarl Mengi naye alikuwepo. Hapa anateta jambo na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyage

 Wabungewateule, Dk. Faustine  Ndungulile wa Kigamboni na Nape Nnauye wa Mtama wakipongezana baada ya kukutana kwenye hafla hiyo
 Nape akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai kwenye hafla hiyo
 Wajumbe wa iliyokuwa Kamati ya Kampeni za CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi, Abdallah Bulembo na Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Mama Zakiah Meghji wakisalimiana kwa bashasha na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye ni Mbunge Mteule wa Mtama wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa wakati wa hafala hiyo
Mwenyekiti wa IPP Reginald Mengi akimsikiliza kwa makini Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi Nape Nnauye wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya viongozi wa CCM, wakiwa kwenye hafla hiyo
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula akisalimia baadhi ya viongozi baada ya kuwasili kwenye hafla hiyo
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akizungumza jambo na Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue wakati wa hafla hiyo
Baadhi ya viongozi mashuhuri wakiwa kwenye hafla hiyo
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jai Mstaafu Sinde Warioba, akiwa na Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, John Malecela wakati wa hafla hiyo
Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Pius Msekwa akizungumza na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi wakati wa hafla hiyo. Wengine ni Spika wa Bunge anne Makinda na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
 Rais Mteule wa Tanzania, Dk. John Magufuli (kulia), akiwapungia mkono wananchi wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiwa cheti cha urais. Kutoka  kushoto ni mgombea urais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira na mgombea nafasi hiyo kupitia Chama cha ADC, Chief Lutalosa Yemba.
 Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi (kushoto), akimpongeza Rais Mteule wa Tanzania Dk. John Magufuli baada ya kuchaguliwa kuwa rais.
 Makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakishangilia wakati Rais Mteule wa Tanzania Dk.John Magufuli alipokuwa akitoka Ukumbi wa Diamond Jubilee kukabidhiwa cheti cha urais.
 Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo.
  Rais Mteule wa Tanzania, Dk.Magufuli akimuonesha Rais Jakaya Kikwete cheti cha ushindi.
 Rais Mteule wa Tanzania, Dk.Makufuli akiwa katika picha ya pamoja na wagombea urais wenzake wa vyama vingine.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpongeza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva kwa kusimamia vizuri uchaguzi mkuu wa 2015.
Rais Jakaya Kikwete na Rais Mteule Dk.John Pombe Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja na wake zao kwenye hafla hiyo.
***************************************
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imemkabidhi cheti cha ushindi aliyekuwa mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk, John Magufuli baada ya kushinda kwa kura nyingi kuliko wenzake kwenye uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Aidha wanasiasa wamemtaka Dk. Magufuli kutekeleza mambo yote ambayo ameahidi, huku Mgombea Urais wa ACT-Wazalendo Anna Mghwira., akimtaka ahakikishe kuwa Katiba ya wananchi inapatikana ili kufanikisha dhana ya mabadiliko ambayo yalikuwa yanatajwa na wagombea wote.

Akizungumza kabla ya kumkabidhi cheti hicho katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam leo Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva, alisema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki huku akiwapongeza wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura tofauti na mwaka 2010.
Lubuva alisema katika uchaguzi huo wagombea wa nafasi ya urais ni Anna Mghwira wa ACT, Chief Lutalosa Yemba wa ADC, Dk. Magufuli wa CCM, Edward Lowassa wa Chadema, Hashim Rugwe wa Chaumma, Malik Kasambala wa NRA, Elifatio Lyimo wa TLP na Fahmi Dovutwa wa UPDP.

Alisema, tume imemtanga Dk. Magufuli kwani amefanikiwa kupata kura nyingi kuliko wagombea wenzake ambapo  walioandikishwa ni wapigakura 23,161,440, waliopiga kura ni 15,589,639 sawa na asilimia 67,31 ya waliojiandikisha.
Alisema kura halali ni 15,193,862 sawa na asilimia 97.46, kura zilizokataliwa ni 402,248 sawa na asilimia 2.58.
Jaji Lubuva alitangaza matokeo kuwa Mghwira amepata kura 98,763 sawa na asilimia 0.65, ADC amepata kura 66,049 sawa na asilimia 0.43.
Dk. Magufuli amepata kura 8,882,935 sawa na asilimia 58.46 sawa na asilimia 58.46, Lowassa amepata kura 6,072,848 sawa na asilimia 39.97, Rungwe 49,256 sawa na asilimia 0.32, Kasambala amepata kura 8,028 sawa na asilimia 0.05.

Wengine ni Lyimo amepata kura 8,198 sawa na asilimia 0.05, Dovutwa amepata kura 7,785 sawa na asilimia 0.05.

Kailima
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uchaguzi, Kailima Ramadhan, alisema kura zilizopigwa zinatoka katika majimbo ya uchaguzi 264 na kata 3,957 na hakuna dosari kubwa ambayo ilitokea.
Alisema katika nafasi ya ubunge majimbo yaliyofanya uchaguzi ni 256 huku majimbo nane yakiwa hayajafanya uchaguzi kutokana na sababu mbalimbali ambazo ni vifo kwa wagombea na karatasi za wagombea kuwa na mapungufu.

Kailima alisema pia kuna Kata ambazo hazijafanya uchaguzi kutokana na mapungufu mbalimbali ambapo wanatarajiwa kufanya uchaguzi mapema iwezekanovyo.
"Mchakato  wa uchaguzi umefanyika kwa kufuata sheria hivyo tume inadiriki kusema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki kwani hakuna lalamiko lolote kutoka kwa wakala," alisema.
Alisema kifungu cha 85 kinaipa mamlaka haki ya kutangaza matokeo hata kama baadhi ya wagombea watagoma kusaini matokeo husika hivyo aliyetangazwa na tume ndiye mshindi.

Mghwira
Akizungumza baada ya tume kumkabidhi mshindi cheti, aliyekuwa mgombea wa urais kupitia ACT-Wazalendo, Anna Mghwira, alisema anakubaliana na matokeo na kumtaka Magufuli ahakikishe kuwa anasimamia upatikanaji wa katiba.

Mghwira alisema, iwapo anataka mabadiliko yaweze kupatikana ni jukumu lake kusimamia upatikanaji wa katiba ya wananchi kwani ndiyo inaweza kuleta mabadiliko sahihi kwa Tanzania ya leo.

Aidha, alimtaka mshindi huyo wa nafasi ya urais kusimamia suala la usawa na umoja wa kitaifa ambao utaweza kujenga nchi kufikia maendeleo sahihi pamoja na wananchi.

"Tunahitaji uchumi imara ili kurejesha fahari ya nchi na wananchi kwani hakuna shaka kuwa wananchi wamekata tamaa na taifa lao jambo ambalo sio sahihi," alisema.

Mghwira alitumia nafasi hiyo kumkabidhi Dk. Magufuli, ilani ya chama hicho kwani ina malengo ya kuibadilisha Tanzania.

Yemba
Kwa upande wake aliyekuwa mgombea urais, kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Chifu Litalosa Yemba, alisema anampongeza Dk. Magufuli kwa ushindi huku akiweka bayana kuwa tangu aanze kushiriki chaguzi uchaguzi wa mwaka huu ndio uchaguzi ambao ulikuwa huru na wa haki.

Alisema mapungufu ambayo yanalalamikiwa na baadhi ya wagombea yanapazwa kuangaliwa kwa undani zaidi ili kuhakikisha kuwa hayarejei kutokana na ukweli kuwa mchakato huo ni muhimu kwa wananchi.

Yemba alisema, anampongeza mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, kwa kufanya kampeni za kistaarabu pamoja na matusi, kashfa na dharau ambazo zimejitokeza kwake.

"Tunaweza kusema mambo mengi ila ambaye ahataki kutambua mchango wa Lowassa katika siasa za Tanzania hasa upinzani atakuwa hajui siasa ninachoomba Chadema na vyama vya upinzani kudumisha nguvu hii kwani hatujaweza kupata kura zaidi ya milioni 2 tangu kuanza kwa vyama vyetu," alisema.

Aidha, ameweka bayana kuwa iwapo angefanya kampeni katika uchaguzi huu angeweza kuwa mshindi wa pili lakini kutokana na uhaba wa fedha walishindwa kufanya kampeni ila anawashukuru wananchi kwa kura ambazo wamepata.

Jonatha
Akizungumzia uchaguzi huo Kiongozi wa waangalizi kutoka Jumuia ya Madola, Rais mstaafu wa Nigeria, Godluck Jonathan, alisema uchaguzi ulikuwa huru na haki na kuzitaka nchi zingine kuiga Tanzania kwani imekuwa mfano bora.

Godluck alisema, uchaguzi ni jambo ambalo linakuwa na changamoto mbalimbali ambapo sio jambo rahisi kila mtu kukubaliana na matokeo lakini kwa mtazamo wao wanaamini kuwa uchaguzi huo umefanyika vizuri.

Nchemba
Mwigulu Nchemba ambaye ni mbunge mteule wa Jimbo la Iramba Magharibi, alisema amefurahishwa na ushindi huo kwani Dk. Magufuli ana vigezo vyote vinavyohitajika kwa kiongozi wa nchi.

Alisema watanzania wajiandae kwa kupata mabadiliko sahihi ambayo walikuwa wanayataka kwani kiongozi huyo ni mtu ambaye anasimamia uwajibikaji, uadilifu na mchapakazi.

"Vigezo vimetumika kumpata rais sahihi kwa maslahi ya Taifa, hivyo kilichobakia ni watu kufanya kazi ili dhana nzima ta hapa kazi tu ionekane na mabadiliko pia," alisema.

Mwijage
"Huyu ndiye chaguo sahihi kwa maslahi ya Taifa na pia naamini hata Mungu ndiye aliyetaka tumpate Magufuli naamini mabadilikio yataanza vijijini ili kuzuia watu kuja mijini kutafuta kazi," alisema.

Alisema watu wajiandae kufanya kazi kwani kasi ya kiongozi huyo mpya wa nchi itakuwa haina mzaha hivyo wale wakaa vijiweni watambue kuwa nafasi hiyo haipo kupitia Dk. Magufuli.

Madabida

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, alisema ushindi huo wameupokea kwa furaha pamoja na ukweli kuwa yalikuwa ndio matarajio yao.

"Sisi hatukuwa na shaka kuhusu ushindi huo lakini pia mgombea wetu ni mtu mzuri sana katika utendaji naamini kuwa wananchi wamemuelewa hivyo watarajie kuona mabadiliko ya kweli," alisema.

Madabida alisema vyama vya upinzani vilikuwa vinatumia nguvu ya hali ya juu kuhakikisha kuwa vinashinda lakini kutokana na mikakati yao wamefanikiwa kuibuka kidedea.

Kuhusu majimbo mengi ya mkoa wake kuchukuliwa na vyama vya upinzani alisema hayo ni maamuzi ya wananchi lakini wao kama uongozi walifanya kila linalowezekana kufanikisha ushindi.

Aidha, alikanusha taarifa za kuwa wameshindwa kutokana na yeye kumuunga mkono Lowassa wakati yupo CCM na kuwa hakufanya kampeni na kuweka bayana kuwa alikuwa anamuunga mkono wakati huo ila kwa sasa alikuwa na Magufuli.

Katika hafla hiyo ya kumkabidhi cheti cha ushindi Dk. Magufuli na Makamu wake Samia Suluhu Hassan, pia Rais Jakaya Kikwete, alishiriki, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Spika wa Bunge Anne Makinda, Rais wa Awamu ya Pili, Ally Hassan Mwinyi, Mawaziri Wakuu wastaafu na viongozi wengine walihudhuria pamoja na wananchi na wanachama wa CCM.
Hali ya meza kuu ya Viongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na waliokuwa wagombea wa Urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 2015, ilivyokuwa kabla ya shughuli kuanza
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishauriana jambo na mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete meza kuu.
Rais Mteule, Dk. John Magufuli akiondoka kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee baada ya kukabidhiwa cheti chake cha kushinda Urais
Mama akiwa na mtoto wake wote wakiwa wamevalia nguo za CCM, wakati wa mapokezi ya Rais Mteule Dk. John Magufuli kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akizungumza kumkaribisha Rais Mteule, Dk. John Magufuli kuzungumza na hadhara kwenye sherehe fupi ya mapokezi iliyofanyika leo kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam
Rais Mteule Dk. John Magufuli akizungumza na wananchi katika mapokezi yaliyofanyika leo kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam
Wananchi waliompokea Rais Mteule Dk. John Maguli wakishangilia wakati wa mapokezi hayo Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam
Wananchi waliompokea Rais Mteule Dk. John Maguli wakishangilia wakati wa mapokezi hayo Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam
Rais Mteule Dk. John Magufuli akiwahutubia wananchi hao
Makamu wa Rais Mteule, Mama Samia Suluhu Hassan, akionyesha cheti chake cha ushindi
Dk. John Magufui akizungumza na wananchi huku akiwa na Makamu wake wa Rais Mteule Mama Samia
Rais Mteule wa Tanzania, Dk. John Magufuli akimtambulisha mkewe, Mama Janneth Magufuli wakati wa hafla hiyo.
Rais Jakaya Kikwete akiwa na Rais Mteule Dk. John Magufulu wakati wa hafla hiyo
Rais Jakaya Kikwete akiwa na Rais Mteule Dk. John Magufulu wakati wa hafla hiyo ya mapokezi iliyofanyika leo kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.