Habari za Punde

*TAIFA STARS YAANZA VYEMA KUFUZU MAKUNDI KOMBE LA DUNIA, YAIBAMIZA MALAWI 2-0

TIMU ya Taifa ya Tanazania, Taifa Stars, leo imewapa raha watanzania kwa kuibuka na ushindi wa kwanza kwa mwaka huu, baada ya kuwaadhibu Wamalawi kwa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza wa mchujo kuwania kupangwa makundi ya kuwania tiketi ya Kombe la Dunia linalotarajia kufanyika nchini Urusi mwaka 2018.

Ikumbukwe kuwa tangu kuanza kwa mwaka huu, Taifa Stars imeshacheza jumla ya mechi 11 bila ya kupata ushindi kwa mwaka huu, na kati ya hizo mechi nane wakiwa chini ya kocha, Mholanzi, Mart Nooij, aliyetupiwa virago, ambapo kwa ushindi wa leo Stars, imejiweka katika nafasi nzuri ya kusonga hatua ya mwisho ya mchujo, ikitarajia kukutana na miamba wa soka wa Algeria, iwapo wataibuka na ushindi wa marudiano wa  ugenini na Malawo utakaopigwa siku ya Jumapili, jijini Blantyire.
Mchezo wa leo ulichezeshwa na Hagi Yebarow Wiish aliyesaidiwa na Hamza hagi Abdi na Salah Omar Abubakar wote wa Somalia.
Mabao  ya Taifa Stars yalipatikana katika kipindi cha kwanza ambayo yalidumu hadi kumalizika kwa dakika 90 za mchezo, yakifungwa na washambuliaji wa TP Mazembe ya DRC, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta.
Bao la kwanza lilifungwa na Mbwana Samatta katika dakika ya 18 baada ya kumlamba chenga kipa wa Malawi, Simplex Nthala, akiitendea haki pasi nzuri ya pachwa wake Thomas Ulimwengu kutoka upande wa kulia.
Na la pili likatupiwa katika dakika ya 22 na Ulimwengu, aliyeuwahi mpira uliotemwa na kipa Nthala kufuatia krosi ya beki wa kushoto, Mwinyi Hajji Mngwali.
Kipa Ally Musafa Mtinge ‘Barthez’ aliokoa michomo miwili ya hatari ya Malawi kipindi cha kwanza, mmoja wa John Banda na mwingine wa Robin Ngalande.   
Kipindi cha pili, Malawi inayofundishwa na mzalendo pia, Ernest Mtawali ilibadilika na kukataa kuruhusu mabao zaidi.
Kwa mara nyingine, kipa Ally Barthez aliokoa michomo miwii ya hatari kipindi cha pili, wakati makali ya safu ya ushambuliaji wa Stars kipindi hicho yakiwa yamepungua.
Ushindi huo ni zawadi tosha kwa Kocha mzawa ikiwa ni siku moja tu baada ya Mkwasa kusiani Mkataba wa mwaka na nusu Taifa Stars, na wa kwanza tangu aanze kazi Julai baada ya mechi nne, akitoa sare mbili 1-1 na Uganda, 0-0 na Nigeria na kufungwa 2-1 na Libya.
KIKOSI CHA TAIFA STARS:  Ally Mustafa ‘Barthez’, Shomary Kapombe, Mwinyi Hajji, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Himid Mao, Thomas Ulimwengu/Ibrahim Hajib dk86, Said Ndemla, Mbwana Samatta, Mrisho Ngassa/Salum Telela dk69 na Farid Mussa/Simon Msuva dk80.

KIKOSI CHA MALAWI: Simplex Nthala, Stanley Sanudi, Mivale Gabeya, Yamkani Fadya, Limbikani Mzava, Gerald Phiri, Chimango Kayira, Micium Mhone/Mamase Chiyasa dk46, Chawangiwa Kawanda, John Banda/Gabadinho Mhango dk58 na Robin Ngalande. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.