Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue
akizungumza leo jijini Dar es salaam katika mkutano wa wadau wa takwimu uliondaliwa
na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wenye lengo la kujadili na kukubaliana jinsi
ya kutekeleza mpango wa Maendeleo Endelevu (SDGs).
Mkurugenzi Mkuu wa
Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa akizungumza katika mkutano wa
wadau wa takwimu uliondaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wenye lengo la
kujadili na kukubaliana jinsi ya kutekeleza mpango wa Maendeleo Endelevu
(SDGs).
Mwakilishi makazi wa
benki ya dunia nchini Tanzania Ms. Bella bird akizungumza leo jijini Dar es
salaam katika mkutano wa wadau wa takwimu uliondaliwa na Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS) wenye lengo la kujadili na kukubaliana jinsi ya kutekeleza mpango
wa Maendeleo Endelevu (SDGs).
Baadhi
ya wadau wa takwimu wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni
Sefue katika mkutano wa wadau wa takwimu uliondaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu
(NBS) wenye lengo la kujadili na kukubaliana jinsi ya kutekeleza mpango wa
Maendeleo Endelevu (SDGs).
****************************************
Na
Mwandishi Wetu, Dar
es Salaam
KATIBU Mkuu Kiongozi,
Balozi Ombeni Sefue amesema Tanzania ina nafasi kubwa ya kufanikisha malengo ya
Mpango wa Maendeleo Endelevu (SDGS).
Akizungumza na wadau
wa Takwimu kwenye mkutano ulifanyika leo jijini Dar es salaam, Sefue amesema
kutokana na Tanzania kufanya vizuri katika utekelezaji wa Malengo ya Milenia
(MDGS) unaokamilika mwaka huu, ni hali inaoyonyesha kwamba Mpango huu mpya wa Maendeleo
Endelevu utatekelezeka kwa ufanisi mkubwa.
“Leo hii tupo hapa kwa pamoja kukubaliana ni
jinsi gani tutaweza kufanikisha mpango mpya wa Maendeleo Endelevu (SDGs) baada
ya kumalizika kwa utekelezaji wa Malengo ya Milenia (MDGs) ambao nchi yetu kwa
kiasi kikubwa tumefanya vizuri,”amesema Sefue.
Sefue ameongeza kuwa,
utekelezaji wa mpango huo mpya unahitaji uwepo wa takwimu za uhakika ambapo
Tanzania inaendelea kuiboresha na kuiwezesha Ofisi ya Taifa ya Takwimu ili
iendelee kutoa takwimu rasmi zitakazowezesha kupima utekelezaji wa mpango huu.
Sefue alisema utekelezaji
wa mpango huu wa Maendeleo Endelevu kwa awamu hii unahitaji kila nchi kutoa
ripoti ya utekelezaji wake kwa mwaka na hivyo itasaidia kufuatilia mafanikio
ama changamoto zake kwa ukaribu.
Aidha, Sefue alisema kufanikiwa
kwa Malengo Endelevu kutasaidia kuboresha maisha ya watanzania kutokana na
malengo 17 yaliyopo kwenye mpango huo mpya kujikita katika uimarishaji wa hali
ya maisha ya wananchi kwa ujumla.
Kwa upande wake Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Prof. Adolf Mkenda amesema kupitia Wizara ya
Fedha, Serikali itahakikisha inaweka kipaumbele cha bajeti katika kufanikisha utekelezaji
wa mpango huo.
“Tanzania imejipanga
vizuri na kama ambavyo tulifanikiwa kutekeleza Malengo ya Milenia, tutatekeleza
pia malengo haya mapya na kuboresha maisha ya wananchi wetu,” alisema Prof.
Mkenda.
Mwezi Septemba mwaka
huu, viongozi wa nchi mbalimbali duniani akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, walikutana nchini Marekani kwa ajili ya kutathmini
utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia – MDGs ambapo ilionekana kwamba
kuna baadhi ya malengo yalikuwa yamefanikiwa na mengine hayakufanikiwa.
Kutokana na hali hiyo,
viongozi hao walikubaliana na kuridhia mpango mbadala wa MDG unaoitwa Mpango wa
Maendeleo Endelevu ambao pia ni wa miaka 15 kuanzia 2015 hadi 2030 ambao
Tanzania imeanza kuufanyia kazi.




No comments:
Post a Comment