Askari wa JWTZ wakiwa kwenye mazoezi ya paredi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya sherehe za kuapishwa Rais mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli na Makamu wake, Samia Suluhu, keshokutwa Nov 6 siku ya alhamihamisi kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Jukwaa linavyoonekana
Kibanda cha kitakachotumika wakati wa kuapishwa kwa Rais Mteule, Dk John Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kesho kutwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Askari wa Jeshi la Wananchi akiigiza kama Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange na mwingine akiigiza kama Rais anayemaliza muda wake, Jakaya Kikwete wakati wa mazoezi ya sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange (wa pili kulia), Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Maangu (wa tatu kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick wakipiga saluti ulipokuwa unaimbwa wimbo wa Taifa wakati wa mazoezi ya sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kikundi cha sarakasi kikitumbuiza wakati wa maandalizi hayo
Wasanii kutoka Zanzibar wakicheza ngoma ya kibati wakati wa mazoezi hayo
Mtu aliyeigiza kama Rais Jakaya Kikwete, akiwa amesimama alipokuwa akipigiwa mizinga ikiwa ni ishara ya kuagwa kwa rais huyo kabla ya kuapishwa Rais mpya wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli wakati wa mazoezi hayo.
Mtu aliyeigiza kama Rais Jakaya Kikwete, akielekea kukagua gwaride la heshima la kumuaga wakati wa mazoezi hayo.
No comments:
Post a Comment