Habari za Punde

*MASHINDANO YA MISS UNIVERSE TANZANIA 2015 KUANZA RASMI

Mashindano ya kumsaka mrithi wa Taji la Miss Universe Tanzania 2015 linaloshikiliwa na Caroline Bernard, yameanza rasmi.

Mpaka sasa tayari waandaaji wameanza kupokea fomu na picha za warembo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania na Visiwani Zanzibar.

Miongoni mwa mikoa ambayo Miss Universe Tanzania imepokea na inaendelea kupokea fomu na picha za washiriki ni  Arusha, Mwanza, Tanga, Iringa, Mbeya na Dar es Salaam. Zoezi la usaili na kupokea fomu kutoka mikoani litahitimishwa siku ya Jumamos kwa kufanya usaili hapa Dar es salaam katika ukumbi wa King Solomon’s uliopo Kinondoni mkabala na Best Bite.

Warembo wote wenye sifa wanaombwa wajitokeze hata kama bado hawajachukua fomu kwani ukiondoa kugombania taji kubwa la Miss Universe Tanzania pia washindi wa pili na wa tatu hupata fursa ya  
kushiriki katika mashindano mengine madogo ikiwemo Miss Earth kwenda kushindana kimataifa kama wenzao waliotangulia.

Mashindano ya Miss Universe kwa hapa Tanzania yalianza rasmi mwaka 2007 ambapo Tanzania iliwakilishwa na Flaviana Matata na kufanikiwa kuingia katika kumi bora na mwaka 2008 yaliwakilishwa na Amanda Ole  
Sulul, mwaka 2009 Miss Universe Tanzania iliwakilishwa na Illuminata James,ambapo mwaka 2010 alikuwa ni Hellen Dausen, mwaka 2011 Nelly Kamwelu, mwaka 2012 Winfrida Dominic, mwaka 2013 Betty Omara ndiye  aliyepeperusha bendera ya Tanzania na mwaka 2014 ni Caroline Bernard ambaye ndiye anayekabidhi taji mwaka huu

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.