Habari za Punde

*FELIX NA WINFRIDA WALIVYOMEREMETA MWISHONI MWA WIKI

 Bwana Harusi Felix, akimvisha Pete ya Ndoa mkewe, Winfrida, wakati wa FELISherehe yao iliyofanyika kwenye Ukumbi wa River Side Ubungo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita. Maharusi hao walifunga ndoa yao takatifu kwenye Kanisa la SDA Mwenge Desemba 13, 2015.
 Wanandoa hao wakifungushwa ndoa na Mchungaji wa Kanisa la SDA Mwenge.
 Bwana Harusi akifurahia huku akimfunua mkewe na kuhakikisha kuwa hajabadilishiwa na wala hajauziwa mbuzi kwenye gunia.....
 Maharusi haowakilishana Keki kama ishara ya upendo wakati washerehe ya ndoayao kwenye Ukumbi wa River Side Ubungo,jijini Dar.
 Maharusi hao wakipozi kwa picha baada ya kutoka Kanisani kufunga ndoa....
 Daaah........Mahaba Niue.....Bwana harusi akimvisha Kiatu mkewe, yaani maupendo haya yaendelee yasiishie siku hii pekee.
 Wasimamizi wa kiume wa sherehe hiyo wakipiga picha ya kumbukumbu na Bi Harusi....
 Maharusi wakipozi kwa picha ukumbini....
 Mc wa sherehe hiyo (kulia mbele) akimpa shavu kujitangaza Mkurugenzi wa Kampuni ya Mafoto Production Sufianimafoto, aliyekuwa akitoa huduma ya Video Live na Picha za mnato katika sherehe hiyo.
 Hapa me sikumuelewa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo kwamba alikuwa akijipanga kumfumua Matron kwa makaratee au ilikuwa ni miondoko ya Ekodteee,.....
 Mc wa sherehe hiyo akigonganisha glasi na maharusi...
 Bi harusi Winfrida akimvisha pete ya ndoa mumewe, Felix....
 Mc akifanya yake kuendesha sherehe hiyo.....
 Bwana na Bi Harusi wakijiachia wakati wakiingia ukumbini kwa miondoko ya kwaito....
Mc akifanya yake kwa staili ya kufungua shampein huku akisebeneka na Ekodteeee, ekodteeee..

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.