Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu
Hassan, akizungumza na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Hanne-Marie
Kaarstad, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Dec 11,
2015 kwa mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu
Hassan, akiagana na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Hanne-Marie
Kaarstad, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Mhe Makamu, Ikulu
jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Samia Suluhu
Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Hanne-Marie
Kaarstad (kulia kwake) na Mkurugenzi wa
Idara ya Ulaya na Marekani, Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine (kulia) na Msaidizi wa Balozi
(kushoto) mara baada ya mazungumzo ao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan,
akizungumza na Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Mhe. Hawa Ndilowe, wakati
alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, jana Dec 10, 2015 kwa
mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Samia Suluhu
Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Mhe. Hawa
Ndilowe baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,jana.
**************************
TAARIFA
KWA UMMA
MAKAMU
WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA
MABALOZI WA NORWAY NA MALAWI
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana
amekutana na Balozi wa Malawi nchini Tanzania na kufanya naye mazungumzo
yaliyolenga kukuza uhusiano wa nchi hizi mbili, sambamba na kuongeza tija ya
maendeleo huku wakifahamishana nia ya kuwa na miradi ya pamoja itakayolenga
kuongeza uhusiano wa pamoja na kupunguza changamoto zinazozikabili nchi hizi.
Katika
hatua nyingine, Mheshimiwa Makamu wa Rais leo Desemba 11, 2015 amekutana na
Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mheshimiwa Hanne-Marie Kaarstad ofisini kwake
Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo walizungumzia kuhusu uongezaji wa mahusiani
na ushirikiano hasa katika suala la mazingira. Balozi Kaarstad ni mpya nchini
Tanzania na ujio wake ameelezea kuwa unalenga katika kuongeza tija kwa nchi
hizi mbili na kwamba Norway itabakia kuwa rafiki wa karibu wa Tanzania.
Imetolewa
na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Ikulu,
Dar es Salaam





No comments:
Post a Comment