Habari za Punde

*MISS UNIVERSE 2015 LORRAINE MARRIOT AKIWA MASHINDANONI LAS VEGAS - NATIONAL COSTUME

Miss Universe Lorraine akiwa katika vazi la ubunifu la Taifa . Vazi hili limebuniwa na Adam Hassana Kijangwa kutoka Zanzibar na limeitwa 'Angel of Ivory' kutokana na muonekano wake wa kuonyesha Malaika wa Tanzania anayelinda Tembo wanaouwawa kwa ujangili kwa ajili ya biashara haramu ya pembe za ndovu.
Huyu malaika wa Tanzania yupo kwa ajili ya kuwalinda Tembo na rasilimali zetu na kuwaadhibisha majangili. Nguo yake imeshonwa kwa ubunifu na umahiri mkubwa na hekaheka limebuniwa na Mwanakombo Salim. Pia kabeba fimbo ya Kimasai iliyonakshiwa na rangi za taifa.
Rangi nyekundu ni alama ya damu ya tembo iliyomwagika na kusafishwa na malaika huyu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.