Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akitangaza Baraza jipya la Mawaziri, wakati wa mkutano na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Dec 10, 2015. Kushoto ni Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan na (kulia) ni Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa. Picha na OMR
******************************************
Na Ripota wa Sufianimafoto, Dar
Baada ya mwezi mmoja nasiku kadhaa, huku kukiwa na kitendawili kuhusu Baraza jipya la Mawaziri, hatimae leo Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ametegua kitendawilihicho kwa kuvunja ukimya na kutangaza Baraza lake jipya la mawaziri.
Akitangaza majina ya Mawaziri hao kwenye Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam, leo mchana Rais Dkt. Magufuli, alisema kuwa amejitahidi kadri awezavyo kupunguza na kuziunganisha baadhi ya Wizara ili kuweza kuendana na kaulimbiu yake ya 'HAPA KAZI TU' na kubana matumizi ambapo amefanikiwa kupata jumla ya Wizara 18 tu kutoka Wizara hamsini na kitu.
“Walioteuliwa wasifikirie kufanya sherehe kwa sababu kazi niliyowapa ni ngumu, ila wajiandae kufanya sherehe wakifukuzwa.” Alisema. huku akicheka
Aidha Rais Magufulia alisema kuwa katika Baraza hilo, hakutakuwa na semina elekezi na kwamba fedha zilizotengwa kwa ajili ya semian hiyo jumla ya shilingi Bilioni mbili, zitaelekezwa kwenye shughuli nyingine za kijamii kama elimu. “ Watajipa semina wenyewe humo humo ndani kama ambavyo Mhe. Waziri Mkuu alivyojipa kwa kwenda kutumbua majipu Bandarini si alijielekeza mwenyewe, Na mimi nilijielekeza mwenyewe na Mhe Samia alijielekeza mwenyewe” alisisitiza.
Baraza hilo jipya la serikali ya awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kama ifuatavyo:- KUSOMA ZAIDI NA KUWAJUA MAWAZIRI HAO BOFYA READ MORE
Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, kutakuwa na mawaziri wawili ambao ni George Simbachawene na Angellha Kairuki, Naibu waziri atakuwa Jaffo Selemani Said, Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano na mazingira, Waziri atakuwa Januari Makamba,na Naibu waziri Luhaga Mpina, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi Vijana Ajira na Walemavu), Jenista Mhagama, naibu waziri, Dkt. Possi Abdallah, naibu waziri mwingine ni Anthony Mavunde, Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchema, Naibu Waziri William Ole Nasha, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Waziri (bado), naibu waziri, Injiania Armandus Ngonyani, Wizara ya Fedha na Mipango, (bado), naibu waziri ni Dkt.Ashantu Kijaji, Wizara ya Nishati na Madini, Waziri ni Profesa Sospter Muhongo, naibu Waziri ni Dkt.Medard Karemagi, Wizara ya Katiba na Sheria, Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe, Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Masharioki, Kikanda na Kimataifa, Dkt. Augustine Mahiga, kuwa Mbunge na ameteuliwa kuwa waziri wa wizara hiyo, Naibu waziri ni Dkt. Suzan Alfions Kolimba, Wizara ya Ulinzi na Jeshio la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Waziri ni Bw. William Lukuvi, Naibu wake ni Bi. Angelina Mabula, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, Naibu wake, ni Injinia Isack Kamwela, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee, Waziri ni Bi. Ummy Mwalimu na Naibu wake ni Dkt. Khamisi Kigwangala, Wizara ya Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Waziri ni Bw. Nape Nnauye na Naibu wake ni Bi. Anastazia James Wambura, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Elimu, (Waziri bado), naibu wake ni Injinia Stella Manyanya, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Waziri ni Bw. Charles Mwijage, Wizara ya Maliasili na Utalii, (Waziri bado), Naibu wake ni Injinia Ramo Makani, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Charles Kitwanga.
Balozi Augustine Mhiga
Dkt. Harrison Mwakyembe
Bw. George Simbachawene
Bi. Angellah Kairuki
Bw. January Makamba
Bw. Nape Nanuye
Profesa Sospeter Muhongo
Dkt. Hussein Mwinyi
Bw. William Lukuvi
Bi. Ummy Mwalimu
Bw. Mwigulu Nchemba
Prof makame mnyaa mbawara.
![]() | ||
![]() | ||
![]() | |||
![]() | ||
| . |


















No comments:
Post a Comment