Habari za Punde

*CYNTA WA 'JUMA NATURE' ASOTA KITUONI OYSTERBAY BAADA YA KUDAKWA AKITANUA KUKWEPA FOLENI

Msanii wa siku nyingi na Mwandishi wa habari, al-maarufu kama Cynta, akiwa kwenye gari lake dogo akitoka Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam,baada ya kusota kuanzia mida ya saa nne asubuhi na hii ilikuwa ni mishale ya saa kumi na dakika zake jioni.
Cynta alidakwa majira hayo na Askari wa usalama Barabarabi pale maeneo ya Ubalozi wa Ufaransa alipokuwa akijaribu kutanua ili kukwepa foleni iliyokuwa imebamba pande hizo.
Akizungumza na mtandao huu mara baada ya kuchomoka Kituoni hapo, Cynta alisema kuwa alidakwa yeye na watu wengine kibao wapatao 40 hivi na kupelekwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay na kuwekwa chini ya ulinzi na baadaye kutakiwa kulipa faini, ambapo baadhi walifanikiwa kulipa na kuachiwa huru.
Lakini pamoja na kulipa faini hizo ieleweke siku hizi ukikamatwa kwa kosa la kutanua utaratibu ni kupelekwa Mahabusu na kisha Mahakamani. Unapigwa picha na kibao mbele ya gari, lako unachukuliwa finger prints na details zako. Ukifanya kosa mara ya pili unafutiwa leseni.  Zoezi hili limeanza rasmi leo, hivyo kuweni makini. 
Barabarani huenda pia Leseni yako ikapunguzwa pointi yaani inawekewa alama ili kuhesabu makosa yako.
Aidha katika tukio jingine lililotokea maeneo ya Kinondoni leo na watuhumiwa kufikoshwa kituoni hapo, ni Baadhi ya abiria waliokuwa wakimzomea Askari wa usalama Barabarani wakati akiongoza magari ya upande mmoja ili kuruhusu Msafara wa Kiongozi Fulani..

Abiria hao baada tu ya kupita msafara huo walianza kumzomea kuhu wengine wakitukana jambo ambalo lilimkasilisha askari huyo na kuamua kulikamata gari hilo na abiria wake na kulipeleka Kituo cha Polisi Oysterbay.

Walipofika Kituoni hapo abiria hao wote walishushwa na kuwekwa chini ya ulinzi na kutakiwa kutajana na ndipo walipotajana na wakapatikana waliokuwa wakitenda kosa hilo Wanawake wanne na Wanaume watatu na kutiwa Mahabusu wakisubiri kupelekwa Mahakamani kesho baada leo kuchelewa.

Hadi Mwandishi wa mtandao huu anaondoka Kituoni hapo watuhumiwa hao walikuwa bado wapo Mahabusu huku wale wa kosa la Kutanua wakiwa bize kuhangaikia kutimiza masharti na Cynta alikuwa akiondoka Kituoni hapo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.