Habari za Punde

*MWILI WA MAREHEMU ASHA BAKARI ALIYEFARIKI DUBAI WAWASILI VISIWANI ZANZIBAR KUZIKWA LEO SAA NNE JANG'OMBE

Mwili wa Marehemu ukiteremshwa katika ndege kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.
Marehemu Asha Bakari alifariki nchini Dubai akitokea Nchini India alikokuwa kwa matibabu. Marehemu anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kianga nje kidogo ya mji wa Unguja na Maiti itasaliwa katika msikiti Mkuu wa Kwamchina saa nne asubuhi. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akizungumza na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Pandu Amaer Kificho na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Mohammed Aboud wakiwa uwanja wa ndege Zanzibar wakisubiri kuwasili kwa mwili wa marehemu
Mwili wa Marehemu ukishushwa katika gari baada ya kupokelewa katika uwanja wa ndege wa Zanzibar. 
Wananchi wakiupokea mwili wa Marehemu Asha Bakari baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Zanzibar baada ya kukabidhiwa na Wafanyakazi wa Uwanja huo. ZAIDI BOFYA READ MORE
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Pandu Ameir Kificho na Viongozi wengine wa Serikali na Vyama vya Siasa na Wananchi wakiuombea dua mwili wa marehemu Asha Bakari baada ya kuwasili Zanzibar. 
Safari ikianza...
Ndugu na Jamaa wakiwa na huzuni baada ya kuupokea mwili wa marehemu.

Wananchi wakishiriki kuombeleza msiba wa marehemu Asha Bakari Makamu Mwenyekiti wa UWT Zanzibar aliyefariki Nchini Dubain wakati akitokea Nchini India katika matibabu.
Ndugu na Jamaa na Wananchi wakishiriki katika dua ya kuuombea mwili wa Marehemu Asha Bakari baada ya kuwasili nyumbani kwa kaka wa marehemu kwa ajili ya matayarisho ya mazishi katika mtaa wa jangombe  
Waombolezaji wakiwa katika msiba jangombe kwa ndugu wa marehemu wakisubiri taratibu za mazishi.
Ndugu wa marehemu wakiomboleza msiba wa ndugu yao nyumbani kwao jangombe Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohammed Aboud akizungumza na Ndg wa c na mareheme baada ya kuwasili kwa mwili wa marehemu Jangombe kwa nduga zake kwa mazishi leo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.