Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Dkt Asha Rose Migiro akimtunuku Shahada ya ya heshima ya udaktari wa falsafa ya mahusiano ya kimataifa Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete katika  maafali ya 30 ya Chuo kikuu Huria Tanzania yaliyofanyika leo Jijini  Dar es Salaam.
 Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wanataaluma na wageni katika  maafali ya 30 ya Chuo kikuu Huria Tanzania yaliyofanyika leo Jijini  Dare s Salaam.
Baadhi ya wahitimu wa shahada mbalimbali  kutoka Chuo kikuu Huria Tanzania.
*****************************************
Na Raymond Mushumbusi Maelezo
Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ametunukiwa Shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa wa mahusiano ya kimataifa Leo Jijini Dar es Salaam katika mahafaliya 30 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania.
Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amesema amefarijika sana kutunukiwa shahada hiyo ya heshima itolewayo na Chuo kikuu Huria Tanzania kwa watu ambao wametoa mchango katika maendeleo katika jamii kupitia nafasi zao kiutendaji.
“Naipokea heshima hii toka Chuo Kikuu Huria Tanzania kwa moyo mmoja kwani wameona mchango ambao nimeutoa nilipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Awamu ya Nne hivyo basi nitaendeleza mahusiano na ushirikiano kimataifa”.Alisema Mhe. Dkt  Kikwete.
Mbali na Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kuna baadhi ya maraisi na wakuu mbalimbali duniani waliwahi kupata Shahada za heshima toka Chuo Kikuu Huria Tanzania ambao ni Rais wa Awamu ya kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Awamu ya tatu Benjamin William Mkapa, Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini Hayati  Nelson Mandela na Dkt Koichiro Mastuura Mkurugenz iwa UNESCO.
Chuo kikuu Huria cha Tanzania kimetoa jumla ya wahitimu 69 wawili Shahada maalum na 67 ni Shahada, Stahahada na Astashahada, ambapo Shahada ya uzamivu ni wahitimu watatu, Shahada ya uzamili ni wahitimu 20, Shahada wahitimu 22,Stashahada wahitimu 15 na Astashahada wahitimu 6.
No comments:
Post a Comment