Habari za Punde

*YANGA WAAREJEA KILELENI MWA LIGI KUU TANZANIA BARA BAADA YA KUIFUNGA NDANDA FC BAO 1-0

 Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma (kulia) akiruka kuwania mpira na beki wa Ndanda Fc, Hemedi Khoja, na (kushoto) ni kipa wa Ndanda, Jeremia Kisubi akiukosa mpira huo wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo yanga ilishinda bao 1-0.
 Beki wa Ndanda Fc, Paul Ngalema, akimdhibiti winga wa Yanga, Simon Msuva.
 Beki wa Yanga, Vicent Bossou, akimtoka mchezaji wa Ndanda Fc....
Beki wa Ndanda Fc Sarvatory Ntebe (kushoto) akiwania mpira na mshambuliaji wa Yanga Amis Tambwe.
 Kocha wa Ndanda Fc, Hamim Mawazo akitoa maelekezo kwa Nahodha wake, Kigi Makassy wakati uliposimama kwa muda mchezo huo.
 Msuva, akichuana kuwania mpira na beki wa Ndanda....
 Msuva akichezewa rafu na beki wa Ndanda....
 Msuva akijaribu kumtoka beki wa Ndanda....
 Wachezaji wa Ndanda wakiwa kwenye Veranda la kuingia vyumba vya kubadilishia nguo vya wachezaji wakati wa mapumziko wakipata maelekezo kwa Kocha wao,ikielezwa kuwa 'Eti' wameogopa hujuma kuingia kwenye vyumba hivyo.
 Kipa wa Ndanda akipangua mpira wa hatari wa kona uliopigwa na Issoufour Abubacar..
Issoufour Abubacar (kulia) akikabwa na mabeki wawili wa Ndanda..
**************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
HATIMAYE timu ya Yanga leo imerejea tena kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara kwenye mchezo wa Ligi Kuu Yanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, jioni ya leo.

Baada ya ushindi wa leo sasa Yanga imefikisha jumla ya Pointi 36 baada ya kucheza mechi 14 sawa na Azam Fc waliorejea nafasi ya pili kwa kutoka sare na African Sports katika mchezo waowa jana.

Bao la Yanga lilifungwa na Kevin Patrick Yondan Dakika ya 60 kwa mkwaju wa penalti kipindi cha pili, huku Amis Tambwe akikosa penati ya kwanza katika dakika ya 47 na baada ya kupatikana penati ya pili wachezaji wote walionekana kuukimbia mpira hadi Kocha alipomwita Nahodha Yondani na kumtaka kupiga penati hiyo.

Hadi sasa Yanga wana jumla ya mabao 31 na kuruhua kufungwa mabao matano pekee, wakati Azam FC ina jumla ya mabao 28 ya kufunga na ya kufungwa tisa, huku wakiwa na pointi sawa na Yanga.

Yanga SC walipoteza nafasi nzuri ya kufunga dakika ya 29, baada ya shuti la mpira wa adhabu la beki wake wa kulia, Juma Abdul kupanguliwa vizuri na kipa wa Ndanda Fc Jeremiah Kisubi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.