Mwamuzi wa mchezo wa Yanga na Majiji, John Fanuel wa Shinyanga akimkabidhi mpira mshambuliaji Amissi Tambwe baada ya kumalizika kwa mchezo huo na kupiga hat trick, wakati Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 5-0 kwenye Uwanja wa Taifa.
********************************************************
YANGA SC imekaa tena kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada kufuatia ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Majimaji ya Songea katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, jana jioni.
Ushindi huo unaifanya Yanga SC kufikisha jumla ya pointi 39, sawa na Azam FC wanaorudi nafasi ya pili wakitofautiana wingi wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Mabao ya Yanga yalifungwa na mshambuliaji Mrundi Amissi Joselyn Tambwe aliyefunga mabao matatu, wakati Wazimbabwe, kiungo Thaban Kamusoko na Mshambuliaji Donald Ngoma wakifunga bao moja kila mmoja.
Bao la kwanza lilifungwa na Kamusoko katika dakika ya nne, akimalizia krosi ya kiungo Deus Kaseke.
Bao la pili lilifungwa na Ngoma kipindi cha pili dakika 47 kabla ya Tambwe kufunga mara tatu mfululizo dakika za 57, 82 na 84.
Katika viwanja vingine huko Mkoani Shinyanga nao Mwadui FC walitakata kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mwadui Complex, African Sports ililazimishwa sare ya 0-0 na Mtibwa Sugar Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Wachezaji wa Yanga wakipongezana.......
Amis Tambwe akiwachachafya mabeki wa Majimaji.....
Kamusoko akipongezana na Tambwe baada ya kutupia...
Donald Ngoma akiruka kukwepa kwanja la Kiungo wa Majimaji, Lulanga Mapunda.
MATOKEO YA MECHI NYINGINE
Yanga SC 5-0 Majimaji
Mwadui FC 2-1 Kagera Sugar
African Sports 0-0 Mtibwa Sugar
Mwadui FC 2-1 Kagera Sugar
African Sports 0-0 Mtibwa Sugar
No comments:
Post a Comment