Naibu Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Anastazia James Wambura (kushoto)
akipokea Kamusi kuu ya Kiswahili kutoka kwa Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili
Taifa (BAKITA) Dr. Selemani Sewange alipotembelea ofisi za BAKITA kufahamu
mambo mbalimbali yanayofanywa na Taasisi hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Anastazia James Wambura (kushoto) akikabidhiwa kitabu kiitwacho Furahia Kiswahili kilichoandaliwa na BAKITA alipotembelea ofisi za BAKITA kufahamu mambo mbalimbali yanayofanywa na Taasisi hiyo jana jijini Dar es Salaam. Anayemkabidhi ni Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili Taifa (BAKITA) Dr. Seleman Sewange
***************************************************
Na: Genofeva Matemu
-Maelezo
Watendaji Taasisi ya
Kiswahili Taifa (BAKITA) wametakiwa kijitangaza na kushiriki katika matukio
mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kuhamasisha matumizi la lugha ya Kiswahili
ili kiweze kufahamika na kutumika na mataifa mengine.
Rai hiyo imetolewa na
Naibu Wazari wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James
Wambura alipotembelea ofisi za BAKITA kutambua kazi mbalimbali zinazofanywa na
Taasisi hiyo jana jijini Dar es Salaam.
“Ni vyema kama mtakua
mkiomba nafasi ya kushiriki katika matukio yote yanayofanyika ndani na nje ya
nchi ili muweze kuhamasisha matumizi ya lugha ya Kiswahili kwani ni lugha ambayo
inakua kwa kasi na kutumiwa na watu mbalimbali” alisema Mhe. Wambura.
Akizungumza wakati wa
ziara ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Katibu Mtendaji Baraza
la Kiswahili Taifa Dr. Selemani Sewange amesema kuwa BAKITA imekua ikishiriki katika
Bunge la Afrika na Umoja wa Afrika hivyo kutangaza lugha ya kiswahili kwa
mataifa mengine na kuahidi kuendelea kushiriki katika fursa zote
zitakazojitokeza ndani na nje ya nchi.
Aidha Dr. Sewangi
amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kwa
kuitanganza nchi na lugha ya Kiswahili alipokutana na marais wa Afrika
Mashariki hivi karibuni Mkoani Arusha.
“Lugha ya Kiswahili
itafahamika na kutumika na watu wa mataifa mengine kama itatumiwa na wazalendo
katika matukio ya kimataifa kama alivyofanya Mhe. Magufuli alivyokutana na
Marais wa Afrika Mashariki hivi karibuni” alisema Dr. Sewange
Baraza la Kiswahili
la Taifa ni Taasisi iliyo chini ya Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo
iliyoundwa chini ya sheria namba 27 ya Bunge la mwaka 1967 kukuza na kuendeleza
matumizi ya Lugha ya Kiswahili Tanzania,
kukuhamasisha matumizi ya Lugha ya Kiswahili katika shughuli rasmi na za umma, kuleta
mafanikio makubwa katika matumizi ya Lugha ya Kiswahili na kukataza matumizi
mabovu.


No comments:
Post a Comment