Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma (katikati) akimtoka beki wa Azam Fc, David Mwantika, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara unaoendelea hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini dar es Salaam. Mpaka sasa ni kipindi cha pili na Yanga wanaongoza kwa mabao 2-1. Mabao ya Yanga yamefungwa na Juma Abdul na Donald Ngoma, na la Azam Fc limefungwa na Kipre Tchetche, yote katika kipindi cha kwanza.
Viongozi wa Azam Fc, wakishangilia bao la timu yao.
Beki wa Yanga, Haji Mwinyi akiruka kukwepa kwanja la beki wa Azam, Shomari Kapombe...
No comments:
Post a Comment