Habari za Punde

*AZAM FC NA YANGA SC ZATOSHANA NGUVU

 Deus Kaseke wa Yanga akichuana kuwania mpira na Mudathir Yahya wa Azam Fc, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo timu hizo zimetokata sare kwa kufungana mabao 2-2.

Hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa mabao 2-1 huku Azam wakiwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Farid Mussa,  akimalizia pasi nzuri ya Kipre Herman Tchetche,  katika dakika ya 11 baada ya kuachia shuti lililombabatiza beki wa Yanga Juma Abdul, aliyeusindikiza mpira huo wavuni.

Yanga nao walipata bao la kusawazisha katika dakika ya 28, kupitia Beki wake wa kulia, Juma Abdul, akiunganisha pasi ya Amis Tambwe na kuachia shuti kali lililomshinda kipa wa Azam Fc, Aishi Manula.

Dakika ya 41, Yanga walipata tena bao la kuongoza kupitia mshambuliaji wake wa Kimataifa, Donald Ngoma, akimalizia mpira uliotemwa na kipa baada ya kupangua shuti la Amis Tambwe.

Hadi mapumziko Yanga walitoka uwanjani wakiongoza kwa mabao 2-1.

Kipindi cha pili timu zote zilifany mabadiliko,Azam wakimtoa Farid Mussa katika dakika ya 60 na kuingia, Didier Kavumbagu, na katika dakika ya 68 Yanga alitoka Simon Msuva na kuingia, Geofrey Mwashiuya, na Azam akatoka Himid Mao na nafasi yake kuchukuliwa na Frank Domayo.

Dakika ya 70 Azam Fc,walipata bao la kusawazisha kupitia kwa Nahodha wake John Bocco,aliyeunganisha pasi ya Kipre Tchetche.

Na Yanga walifanya tena mabadiliko katika dakika ya 82,kwa kutoka Amis Tambwe na naafasi yake kuchukuliwa na Pato Ngonyani, Dakika ya 85, Azam nao walifanya mabadiliko kwa kumtoa Ramadhan Singano na nafasi yake kuchukuliwa na Mudathir Yahya.
 Beki wa Yanga,Vicent Bossou (kulia) akichuana kuwania mpira na Ramadhan Singano wa Azam Fc.
 Mashabiki wa Azam Fc, wakishangilia.....
 Bao la pili la Yanga....
 Mtanange ukiendelea.....
Mashabiki wa Yanga na Azam wakichapana kwa kurushiana viti jukwaani...

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.