Na Ripota wa Sufianimafoto, Dar
KIUNGO mahiri wa Simba Awadh Juma leo ameipaisha timu yake na kurejea Kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuifungia bao pekee katika mchezo wa leo dhidi yao na Tanzania Prisons mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Bao hilo lililofungwa katika dakika ya 86 kwa shuti alilopiga akiwa nje ya 18, limeifanya Simba kufikisha jumla ya Pointi 54 na kushika usukani wa Ligi hiyo wakiwa juu ya Mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 50 na Azam Fc wenye Pointi 47.
Hadi sasa Simba tayari wameshacheza mechi 23, Yanga SC walio nafasi ya pili, wakiwa wamecheza mechi pungufu, 21 na Azam FC wakiwa wamecheza mechi 20 na wakiwa nafasi ya tatu.
Ushindi huo kwa timu ya Simba leo ni wa kulipa kisasi baada ya mzunguko wa kwanza kufungwa bao 1-0 na Prisons katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, Mgambo JKT imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mwadui FC ya Shinyanga katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga, wakati jana Mtibwa Sugar imeifunga 2-1 JKT Ruvu Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
Kesho Timu ya African Sports watakuwa wenyeji wa Mbeya City katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

No comments:
Post a Comment