Habari za Punde

*BASI LA LEINA KUTOKA KAHAMA LAPINDUKA KIMARA DAR LAUA NA KUJERUHI

 Basi la Leina, linalofanya safari zake Kahama- Dar, limepata ajali eneo la Kimara Bucha jijini Dar es Salaam, jana usiku na kuua watu kadhaa akiwamo dereva wa basi hilo.
Aidha imeelezwa kuwa basi hilo liliacha njia na kuanguka na dereva wake alibanwa mbavu na kufariki papo hapo huku baadhi ya abiria wakipasuka Vichwa.

Watu kadhaa walijeruhiwa eneo hilo la tukio wakiwamo abiria waliokuwa wakisubiri usafiri kituo cha daladala baada ya kuangukiwa na basi hilo na wengi wakajeruhiwa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.